Aliyejiunganishia
bomba la mafuta nyumbani kwake Samwel Kilanglani(63) amejulikana kuwa
ni mfanyakazi mstaafu wa bomba la kusafirisha mafuta Tanzania na Zambi
(Tazama).
Kilanglani
anatuhumiwa kutoboa bomba la mafuta ya dizeli la Mamlaka ya Bandari
Tanzania(TPA) na kujiunganishia kwenye mantaki mawili yakiwa ndani ya
nyumba yake iliyopo Tungi Kigamboni.
Kaimu
Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Benedict Kitalika amesema
mtuhumiwa huyo alijiunganishia na bomba la TPA kwa njia ya kuchomelea na
kuunganisha moja kwa moja kwenye mantaki yake mawili yaliyochimbiwa
chini ndani ya nyumba yake.
Kitalika
amesema mtuhumiwa alijiunganishia katikati na bomba kuu hivyo mafuta
yanapopelekwa sehemu husika mengine yanaingia kwake hivyo hayafiki kama
yalivyokusudiwa.
"Mafuta
yanaweza yakapelekwa lita 4,000 sehemu husika lakini hayafiki yote
mengine yanaenda kwa mtuhumiwa huyu matokeo yake wanajiuliza haya
mengine yameenda wapi," amesema
Kamanda
wa Kikosi cha Polisi Bandari, Robert Mayalla amesema inavyoonekana huyu
mtuhumiwa alijiunganishia kipindi mabomba hayo yanajengwa kwa kuwa
kipindi hiki isingewezekana.
Amesema bomba hilo amejiunganisha kwa utaalamu wa juu kwa kuwa hayo mabomba yamepitishwa chini ya ardhi.
Wakati
hao wakisema hivyo Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Deusdedit Kakoko amesema
anaandaa ripoti kuhusu tukio hilo na ataitoa saa tisa leo Jumanne.
"Hili ni suala kubwa linalohusu uchumi wa nchi. Ni sawa na mtu kuvamia kambi ya jeshi."
0 comments:
Post a Comment