Home » » PICHA: Tundu Lissu akiwa amesimama kwa miguu kwa mara ya kwanza

PICHA: Tundu Lissu akiwa amesimama kwa miguu kwa mara ya kwanza

Unknown | Wednesday, December 27, 2017 | 0 comments
SeeBait
Hali ya Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu inaendelea kuimarika na ameanza rasmi kufanya mazoezi ya viungo katika Hospitali ya Nairobi nchini Kenya ambako anapatiwa matibabu ya majeraha aliyoyapata baada ya kushambuliwa kwa risasi nyumbani kwake Area D, mjini Dodoma mnamo Septemba 7, 2017.

Picha kutoka Hospitali ya Nairobi imemuonesha Lissu akifanya mazoezi ya kusimma kwa msaada wa madaktari wa hospitali hiyo. Lissu ameanza mazoezi madogo ya kuimarisha misuli ya miguuni ili aweze kutembea.

Akizungumza kutoka Hospitalini hapo, Lissu ambaye pia ni Mwanasheria Mkuu wa Chadema na Rais wa Chama cha Wanansheria Tanganyika (TLS), amesema “Wapendwa wote wiki iliyopita niliwataarifu kwamba  madaktari wangu wamesema nitasimama, nitatembea na nitarudi Tanzania.

“Leo Boxing Day nimeweza kusimama kwa mguu mmoja kwa msaada wa mababa cheza kama inavyoonekana, hatua inayofuata nitawajulisheni.

“Hatua inayofuata ni magongo kesho na nitawajulisheni hatua nyingine katika matibabu yangu accordingly, Wasalaam,”  Mhe. Tundu Lissu.
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

 
Support : Copyright © 2018. AFRICAN NEWS BLOG - All Rights Reserved
Imetengenezwa na Edwin Moshi
Inaendeshwa na AFRICAN NEWS BLOG