Aliyekuwa
Mbunge wa Siha kwa tiketi ya CHADEMA, Godwin Molel amewataka wananchi
wa Siha kutoogopa akisema ametazama mbali hadi kuhama Chama hicho na
kudai kuwa hawatajuta.
Akiwa kwenye Kampeni Longido Mollel amesema amehoji kama CHADEMA hawanunui watu huwa wanapeleka wapi Tsh Milioni 360 za ruzuku wanayopata kama chama kwa mwezi.
Mollel
amesema kwamba; "Niwaambie watu wangu wa Siha. Msiogope. Mliponichagua
kuwa Mbunge nilitakiwa kulitetea taifa na kuitetea Siha. Cheo ni zaidi
ya maslahi ya taifa na Siha. Msiogope nimetazama mbali na nimeona mbali
hivyo hamtajuta. Nataka kuwamba Rais aliyoko madarakani analitetea
taifa".
Godwin
Mollel alijivua ubunge Disemba 14 mwaka huu kwa kusema kwamba; “Nimeona
nia ya dhati ya Serikali CCM kutetea rasirimali za Taifa, nikaona
niweze kujiuzulu nafasi yangu ya ubunge ili niweze kwenda kujiunga kwa
vitendo katika kulinda rasirimali za Taifa letu, aminini watu wangu wa
Siha nimeona mbali katika maamuzi haya".
0 comments:
Post a Comment