Muigizaji
kutoka nchini, Nigeria Ramsey Nouh ambaye alifanya movie moja itwayo
‘King Of Devil’ na marehemu Steven Kanumba, ametua nchini Tanzania wiki
hii kwaajili ya kukutana na wasanii wa Bongo Movies ambapo jana alipata
nafasi na kunywa chai na Mama Kanumba na baadaye kwenda makaburini
kwaajili na ibada.
Wakiwa
makaburini hapo, Ramsey na Mama Kanumba walitumia muda mwingi
kukumbatiana na kulia kwa huzuni jambo lililoteka na kuvuta hisia za
watu wengi.
Mbali
na tukio hilo, Ramsey alizidisha machungu kwa mama huyo baada ya kuanza
kutamka maneno kama anazungumza na marehemu Kanumba ambapo alimueleza
mambo yenye kuumiza.
“Steven, kwa mara ya mwisho tulizungumza sote tukiwa hai lakini leo nimesimama kando yako ukiwa umelala chini ya mchanga hujitambui, kwangu ni zaidi ya msiba na kwa kweli nimeshindwa kuhimili jambo hili, najua huko uliko unaumia sana hususan ukizingatia ukweli kwamba tasnia ya filamu za Kitanzania inakufa,” alisema Ramsey katika mazungumzo yale na Kanumba aliyoyatoa kwa hisia kali hali iliyomsababishia Mama Kanumba maumivu makali.

0 comments:
Post a Comment