Mbunge
wa Momba kwa tiketi ya CHADEMA , Silinde Ernest David amefunguka juu ya
tetesi kuwa kesho na yeye ataongea na waandishi wa habari na kutangaza
kuhamia Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kusema huo ni uzushi na hawezi
kufanya hivyo.
Silinde
ametumia mtandao wake wa Facebook kukanusha taarifa hiyo na kusema kuwa
hawezi kufanya usaliti huo kwani anatambua kuwa Ubunge wake huo
aliupigania kwa gharama kubwa kwani wapo watu walipoteza maisha, wengine
walifungwa huku wengine ndoa zao zikivunjika ili yeye aweze kushinda
nafasi ya Ubunge.
Aidha
Silinde ametoa ahadi kuwa endapo likitokea jambo hilo basi wananchi
waende kuchoma moto nyumba yake na mali zake zote ambazo wanazifahamu
kama kuonyesha msisitiza kuwa hawezi kufanya jambo hilo.
"Uzushi
unaosambazwa juu yangu katika mtandao wa jamiiforums kuwa nitafanya
press kesho ni uongo uliopindukia. Nasema hili likitokea njoo mchome
moto nyumba yangu na mali zangu zote mnazozifahamu. Nafasi ya ubunge wa
Momba niliutafuta kwa gharama kubwa sana na kuna watu walikufa, wengine
walifilisika, wengine wako jela mpaka leo kwa ajili yangu, ndoa
zilivunjika n.k siwezi kusaliti kwa maslahi yangu binafsi ya ahadi ya
cheo, pesa ama kitu kingine" alisema Silinde
Mbali
na hilo Silinde amedai kuwa thamani ya Ubunge haiwezi kushushwa kama
vocha ya simu kuwa ikiisha unaweza kukwangua nyingine na kuweka tena
0 comments:
Post a Comment