Serikali
kupitia Msemaji Mkuu wake, Dkt. Hassan Abbas imesema kuwa kwa mujibu wa
taarifa ya Shirika la Fedha Duniani (IMF) inaonyesha uchumi wa nchi uko
imara ukilinganisha na nchi zilizofanyiwa tathimini.
Dkt.
Abbasi aliyasema hayo mjini Dodoma alipokuwa akiongea na waandishi wa
habari juu ya maoni ya wataalam wa uchumi kutoka IMF ambao wamemaliza
ziara yao hapa nchini Desemba 12, 2017.
“Ripoti
ya IMF inaonesha katika nusu ya kwanza ya mwaka 2017 uchumi umekua kwa
asilimia 6.8, takwimu ambazo ni za juu katika chumi zinazokua kwa kasi
na ikizidi nchi kadhaa zilizofanyiwa tathmini mwaka 2017 zikiwemo za
Ulaya,” alisema Dkt. Abbas.
Aidha,
kutokana na usambazaji mzuri wa chakula mfumuko wa bei ya chakula
ulishuka hadi kufikia asilimia 4.4 ikiwa ni chini ya lengo ambalo IMF
ilitabiri mfumuko ungekuwa asilimia 5.
Aidha
alisema, Serikali imeendelea kulipa madeni ya ndani ambapo mpaka sasa
Shilingi bilioni 900 zimeshalipwa na shilingi bilioni 37 zimelipa madeni
ya watumishi wa Serikali.
0 comments:
Post a Comment