Mamlaka
ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), imesema wakati wa kuelekea sikukuu za
Krismasi na mwisho wa mwaka, mvua kubwa zinatarajiwa kunyesha katika
mikoa ya Mbeya, Songwe, rukwa na Kigoma.
Meneja
wa kituo Kikuu cha Utabiri wa Hali ya Hewa wa TMA, SAmuel Mbuya,
alieleza kuwa mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo ya ukanda wa
Pwani ni zile za kumalizika kwa msimu wa vuli.
Mkurugenzi
Mbuya alieleza kuwa Mikoa hiyo minne iliyotajwa ndiyo inayotarajiwa
kuwa na mvua wakati wa sikukuu na ifikapo mwisho wa mwezi huu, mvua
zinazoendelea kunyesha katika mikoa mbalimbali ikiwamo Dar es Salaam
zitakuwa zimefikia ukingoni.
“Mvua
zinazonyesha maeneo ya ukanda wa Pwani ni zile za vuli na zilianza
Oktoba na zinaisha mwisho wa mwezi huu, si mvua zinazoendelea isipokuwa
tu katika mikoa ya Mbeya, Songwe Rukwa na Kigoma ambako katika msimu huu
wa sikukuu kutakuwa na mvua,” alisema.
Aliongeza
kuwa TMA inatarajia mvua zitaendele kunyesha katika mikoa ya. Kigoma,
tabora, Katavi, Rukwa, Songwe, Mbeya, Ruvuma, Lindi, Dodoma na Singida.
Alisema mvua katika mikoa hiyo zilianza kunyesha Novemba na
zinatarajiwakumalizika mwezi Aprili.
Mbuya
aliwataka wananchi kuendelea kufuatilia taarifa zinazotolewa na TMA
mara kwa mara, ili kupata mwelekeo wa hali ya hewa pamoja na kuchukua
tahadhari mapema.
0 comments:
Post a Comment