Home » » NGUVU YA MWAKA 2017 HAPATOSHI MADIHANI VILLAS LODGE MAKETE TOWN NA CHRIS WAMARY

NGUVU YA MWAKA 2017 HAPATOSHI MADIHANI VILLAS LODGE MAKETE TOWN NA CHRIS WAMARY

Unknown | Friday, December 22, 2017 | 0 comments


Mneja wa kituo cha Redio Kitulo Fm Makete Bw, CONRADI MPILA ametoa wito kwa wana Makete kujitokeza kwa wingi katika tamasha linalokwenda kwa jina la NGUVU YA MWAKA 2017 huku akibainisha kuwa tamasha hilo litasindikizwa na msanii nguli wa bongo fleva CHRIS WAMARY.

Akizungumza na AM BLOG Bw, Mpila amesema tamasha hilo limeandaliwa na kituo cha Redio Kitulo Fm kwa kushirikiana na MADIHANI VILLAS LODGE, 


Aidha tamasha hilo limelenga kutoa Elim kwa jamii hususani katika nyanza mbalimbali kama vile : 
  • kutokomeza mimba za utotoni -Niache Nisome 
  • kupunguza maambukizi mapya ya VVU NA UKIMWI
  • kutokomeza madawa ya kulevywa
  • kuzuiya na kupambana na Rushwa
  • vijana na uchumi
katika hatua nyingine mratibu wa NGUVU YA MWAKA 2017 BW,Aldo Sanga amesema pamoja na elimu kutolewa katika nyanza hizo, pia kutakuwa na tuzo kwa washiriki wa tamasha hilo ,tuzo kwa msanii bora wa mwaka,wimbo bora wa mwaka,video bora ya mwaka,msanii chipukizi bora wa mwaka,mtangazaji bora wa mwaka,mtayarishaji wa vipindi bora wa mwaka,kipindi bora cha mwaka,mfanyakazi bora wa mwaka pamoja na msikilizaji bora wa mwaka.



Ameongeza kwakusema wadau mbalimbali kutoka maeneo tofauti watakuwepo kwaajili ya kufanikisha tamasha hilo.
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

 
Support : Copyright © 2018. AFRICAN NEWS BLOG - All Rights Reserved
Imetengenezwa na Edwin Moshi
Inaendeshwa na AFRICAN NEWS BLOG