Baraza
la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) limesema misa ya Krismasi kitaifa
itaadhimishwa katika Jimbo Katoliki Zanzibar katika Kanisa Kuu la
Mtakatifu Joseph, Minara Miwili.
Taarifa
iliyotolewa leo Alhamisi Desemba 21,2017 na Mkuu wa Idara ya
Mawasiliano Jamii ya baraza hilo, Bernard James imesema misa hiyo
itaongozwa na Askofu wa jimbo hilo, Mhashamu Augustino Shao.
Katika sikukuu hiyo inayoadhimishwa Desemba 25 ya kila mwaka, Wakristo duniani huadhimisha kuzaliwa kwa Yesu Kristo.
Awali,
mratibu wa matukio ya kanisa Tumaini Media, John Leveti amesema
Kardinali Polycarp Pengo ataongoza misa ya mkesha wa Krismasi katika
Kanisa Katoliki la Mtakatifu Maurus, Kurasini jijini Dar es Salaam.
"Askofu
msaidizi wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Eusebius Nzigilwa yeye siku
hiyo ya mkesha, Desemba 24 ataongoza ibada katika Kanisa la Mtakatifu
Joseph," alisema Leveti.
"Siku ya sikukuu Kardinali Pengo atafanya ibada katika Kanisa la Mtakatifu Joseph na Nzigilwa atakuwa St Peters," amesema.
0 comments:
Post a Comment