IKIWA
ni siku moja baada ya taarifa kusambaa mitandaoni kuwa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Mhe Dkt. John Pombe Magufuli ametunikiwa Tuzo
ya Amani ya Mandela (Mandela Peace Prize) huko nchini Afrika Kusini,
huku kukikosekana taarifa rasmi kutoka kwa waandaaji wa tuzo hizo.
Leo
Alhamisi, Desemba 28, 2017 kupitia kipindi cha Joto la Asubuhi cha
Radio E-FM, Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano ya Rais (Ikulu),
Gerson Msigwa amesema kuwa hana taarifa yoyote juu ya tuzo hiyo.
“Mimi
sina taarifa zozote kwa sababu mtu anapotoa tuzo sio lazima awasiliane
na mtu anayempa tuzo, wao wanakuwa na vigezo vyao kadri ya watu
walivyowapima viongozi.“ amesema Msigwa.
“Mimi
sina information zozote kwa hiyo ni vizuri mngewatafuta hao Nelson
Mandela wenyewe hicho chuo waweze kuwaeleza tuzo hizo taarifa wanakuwa
nazo vyuo wenyewe,“ amesisitiza Msigwa.
Hata
hivyo tayari Wakfu wa Nelson Mandela nchini Afrika Kusini umebainisha
kuwa haukuandaa, kusimamia wala kutoa tuzo hizo, ambazo zimeripotiwa
katika vyombo mbalimbali ya habari nchini Tanzania, Kenya na Burundi
jana Desemba 27, 2017.
0 comments:
Post a Comment