Jeshi
la Polisi Mkoani Tabora linawashikila watu watatu akiwemo baba mzazi
wa mtoto Leokadia Maganga, mwenyekiti pamoja na mtendaji wa kata ya
Ndala wilaya ya Nzega mkoani Tabora, kwa tukio la mauaji ya mtoto huyo
mwenye umri wa miaka 11
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Tabora Kamishna Msaidizi Muandamizi wa Polisi (SACP),
Wilbroad Mutafungwa amesema mtoto huyo inadaiwa aliuwawa na
kutumbukizwa kwenye kisima cha maji katika kijiji cha Budushi kata ya
Ndala wilayani Nzega Mkoani Tabora.
"Ni
kweli tulipokea taarifa za tukio hilo la mtoto kukutwa katika kisima
cha maji na baadae kuzikwa, tuliamua kwenda mahakamani kuomba hati ya
kufukua maiti ili tufanye uchunguzi, baba mzazi wa mtoto huyo bado
tunamshikila kwa ajili ya upelelezi", amesema Kamanda Mutafungwa.
Sambamba
na hilo Kamanda Mutafugwa amewaomba wananchi wawe wavumilivu katika
kipindi hiki ambacho Jeshi la Polisi linafanya uchunguzi, ili kubaini
chanzo zaidi cha mtoto huyo kufariki, na mara utakapokamilika watatoa
taarifa zaidi ya tukio hilo.
0 comments:
Post a Comment