Home » » Serikali yatolea ufafanuzi zuio la kufanya Mikutano ya Siasa Nchini

Serikali yatolea ufafanuzi zuio la kufanya Mikutano ya Siasa Nchini

Unknown | Monday, May 07, 2018 | 0 comments
Serikali kupitia Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Antony Mavunde,imesema kwamba haijaweka zuio kwa vyama vya siasa kufanya siasa, bali kuna sheria ambazo zinapelekea kutokea kwa ahli hiyo.

Akijibu swali Bungeni kwa niaba ya Waziri Mkuu, Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Antony Mavunde, amesema seikali haijuzia vyama vya siasa kufanya siasa, kwani imevipa uhuru vyama hivyo kufanya shughuli zake za kisiasa, isipokuwa kuna sheria za jeshi la polisi ndizo zinatoa muongozo juu ya ufanyikaji wa mikutano ya siasa na maandamano.

“"Si kweli kwamba serikali inazuia harakati za kisiasa, sheria imetoa uhuru kwa vyama kutafuta wanachama na kufanya mikutano lakini iko subject na sheria nyinginezo, ikiwemo sheria ya Police force na auxiliary service act ambayo pia imeweka masharti katika section namba 44 na 45 ya namna vyama vya siasa vinaweza vikafanya kazi zao hasa katika mikutano na maandamano mbali mbali”, amesema Anthony Mavunde.

Swali lililojibiwa lililoulizwa na Mbunge wa Rombo Joseph Selasini ambalo lilitaka serikali kusimamia sheria ikiwemo inayowaruhusu wanasiasa kufanya siasa.

Share this article :

0 comments:

Post a Comment

 
Support : Copyright © 2018. AFRICAN NEWS BLOG - All Rights Reserved
Imetengenezwa na Edwin Moshi
Inaendeshwa na AFRICAN NEWS BLOG