Home » » Kauli ya Jaji Mkuu Kuhusu mlundikano wa kesi Mahakamani

Kauli ya Jaji Mkuu Kuhusu mlundikano wa kesi Mahakamani

Unknown | Monday, May 07, 2018 | 0 comments
Jaji Mkuu wa Tanzania, Prof Ibrahimu Juma leo May 7, 2018 amefungua mafunzo elekezi kwa majaji wapya 14 wa Mahakama Kuu nchini yakiwa na lengo la kuwataka wafanye kazi kwa umakini.

Jaji Prof Juma amezindua mafunzo hayo ya wiki 3, katika Kituo cha Mahakama cha Mafunzo ya Uongozi kilichopo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Amesema kuwa Majaji wanatakiwa kutambua kadri wananchi wanavyozitambua haki zao, mlundikano wa kesi unaweza kuongezeka lakini hiyo isiwe kigezo cha wao kushindwa kukidhi matarajio ya wananchi ya kusikiliza mashauri yao na kuyatolea maamuzi kwa wakati.

Akizungumzia mlundikano unaosababishwa na upungufu wa majaji, Jaji Prof Juma amewataka majaji kutumia muda wao vizuri na kujitahidi kuamua kesi ambazo zinaweza kutolewa uamuzi mapema na kumalizika.
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

 
Support : Copyright © 2018. AFRICAN NEWS BLOG - All Rights Reserved
Imetengenezwa na Edwin Moshi
Inaendeshwa na AFRICAN NEWS BLOG