Home » » WANANCHI WAASWA KUTO LALAMIKIA ANKRA ZA MAJI MAKETE

WANANCHI WAASWA KUTO LALAMIKIA ANKRA ZA MAJI MAKETE

Unknown | Friday, April 20, 2018 | 0 comments
Image result for picha ya bomba ya maji
Wananchi wa mamlaka ya mji mdogo wa iwawa wilayani makete mkoani njombe wameaswa kuacha malalamiko kuhusu bili ya maji kuwa kubwa wakati hicho ni  kiwango bora cha ulipaji wa maji kutokana na matumizi ya wanayotumia majumbani mwao.

Akizungumza katika uzinduzi ya  kamati  ya  bodi mpya ya kusimamia huduma ya maji  mamlaka ya mji mdogo wa iwawa[MUWASA] uliofanyika katika ukumbi wa spiricho  makete mjini  kaimu mhandisi wa maji wilaya ya makete NAUMU TWEVE ambaye alikuwa ni mgeni rasmi kwa niaba ya mkuu wa wilaya ya makete mh VERONIKA KESSY amesema kuwa kiwango bili ya maji  kinachotozwa  na mamlaka ya maji mji mdogo wa iwawa ni kizuri kutokana na miundombinu ya mabomba ni gharama huku akiiomba bodi mpya kutoa elimu kwa wananchi kuhusu mgawo wa maji katika mamlaka ya mji mdogo wa iwawa.

FRANCIS NAMAUMBO ni Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya makete amesema kuwa serikali imetoa shilingi milioni mia nne tisini [490] katika mradi wa maji uliopo kijiji cha ivilikinge kata ya isapulano uliokamilika kwa asilimia 75 utakao saidia kutatua changamoto mbalimbali ya malalamiko ya baadhi ya wananchi kukosa maji kata ya iwawa.

Meneja wa mamlaka ya maji mji mdogo wa iwawa bwana YONASI DANIELI NDOMBA amesema bodi imeundwa ina wajumbe  [7] watakao fanya kazi na watendaji wa mamlaka ya maji mji mdogo wa iwawa ili kutoa huduma inayosthili kwa wananchi.

Mwenyekiti mpya wa boda ya mamlaka ya maji mji mdogo wa iwawa Mchungaji EZEKIELI SANGA amewataka wananchi wa kata ya iwawa kutokata mabomba ya maji na endapo wanaona kuna tatizo la maji wawe wanatoa taarifa kwenye mamlaka husika ili kutatua tatizo hilo la upotevu wa maji huku akisema kuwa kama boda watahakikisha wakati wote wananchi wa mamlaka ya mji mdogo wa iwawa wanapata huduma ya maji.


Diwani wa kata ya iwawa mh ASIFIWE LUVANDA ambaye pia mwakilisha wa wananchi katika bodi iliyozinduliwa hii amesema kama diwani atasaidiana na wajumbe wenzake kuhakikisha mabomba ya mamlaka yanakuwa jirani na wananchi ili waweze kupata huduma kiurahisi.
Image result for picha ya bomba ya maji
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

 
Support : Copyright © 2018. AFRICAN NEWS BLOG - All Rights Reserved
Imetengenezwa na Edwin Moshi
Inaendeshwa na AFRICAN NEWS BLOG