Muigizaji na mchekeshaji wa siku nyingi, Amri Athuman maarufu Mzee Majuto, amelazwa tena katika Hospitali ya Tumaini jijini Dar es Salaam, baada ya kuzidiwa.
Mke wa mwigizaji huyo, Aisha Yusufu, ameiambia MCL Digital leo Aprili 23 kwamba mume wake walimpeleka hospitalini hapo leo saa 7:00 mchana.
Aisha amesema kidonda alichofanyiwa upasuaji kimeleta shida, hivyo kumpeleka kwa ajili ya uangalizi zaidi.
Majuto alilazwa hospitalini hapo Januari mwaka huu na kufanyiwa upasuaji wa tezi dume.
0 comments:
Post a Comment