Home » » Diamond, Wema Sepetu, Steve Nyerere wamlilia AGNESS MASOGANGE

Diamond, Wema Sepetu, Steve Nyerere wamlilia AGNESS MASOGANGE

Unknown | Friday, April 20, 2018 | 0 comments
Leo April 20,2018 simanzi kubwa imetawala kwenye tasnia ya muziki wa Bongo Fleva kupoteza video vixen maarufu Agnes Gerald “Masogange” na kwa upande wa mastaa ambao wameonyesha kuguswa na msiba huu ni pamoja na wanamuziki na waigizaji akiwemo Wema Sepetu, Diamond Platnumz,  Steve Nyerere, na wengine.

Aslay Isihaka ameweka picha ya Masongange na kuandika, “Dah mbele yako nyuma yetu sister, safari yetu moja innalillah wainnailah raajiun,”

Huku Naseeb Abdul maarufu ‘Diamond Platnum’ akiweka picha ya mishumaa na maneno, “Rest in paradise Agnes.”

Rajab Kahali ‘Harmonize’ ameweka picha ya Masongange na kusema, “God’s plan  R.I.P. Aggy.

Naye Steven Mengere 'Steve Nyerere’ ameweka picha tatu tofauti za Masogange na kuzungumzia kifo hicho akianza kwa kusema;

“Nimepokea taarifa ya kifo chako kwa mshtuko mkubwa sana. Masogange amka mama Masogange. Staki kuamini.”

Mcheza filamu, Wema Sepetu ameweka picha ya Masongange ikiambatana na maneno, “Innah lillah wa innah illah rajiun... Dah...!


Advertisement
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

 
Support : Copyright © 2018. AFRICAN NEWS BLOG - All Rights Reserved
Imetengenezwa na Edwin Moshi
Inaendeshwa na AFRICAN NEWS BLOG