Home » » Urusi Yaapa Kuyatungua Makombora ya Marekani Iwapo Itaishambulia Syria....Trump Awabeza, Asisitiza Lazima Yapigwe

Urusi Yaapa Kuyatungua Makombora ya Marekani Iwapo Itaishambulia Syria....Trump Awabeza, Asisitiza Lazima Yapigwe

Unknown | Thursday, April 12, 2018 | 0 comments
Baada ya balozi wa Urusi huko Lebanon kusema kuwa majeshi ya Russia yatatungua makombora yoyote yatakayo lenga Syria, Rais wa Marekani Donald Trump amesema Jumatano kuwa Russia iwe tayari, “ kwani makombora hayo yatapigwa nchini Syria,”

“Hamtakiwi kuwa washirika wa Mnyama Anaeuwa kwa kutumia Gesi ya sumu wananchi wake wenyewe na anafurahia!” Trump amesema hayo katika ujumbe wa Twitter wakati Washington ikiendelea kupima namna ya kulishughulikia madai ya shambulizi hilo la silaha za kemikali.

Urusi imesema makombora ya Marekani yanatakiwa kuwalenga “magaidi” na sio “serikali halali” ya Syria.

Msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov pia amesema Jumatano kuwa pande zote zinazohusika katika mgogoro wa Syria wanatakiwa kujizuilia na vitendo ambavyo vitalisambaratisha eneo hilo.

Saa kadhaa baadae, Jeshi la Urusi lilisema kuwa litayaweka majeshi yake huko Douma, eneo ambako shambulizi la kemikali linashukiwa kutokea Jumamosi ambalo liliuwa watu wasiopungua 40. Urusi imesema majeshi yake yataendelea kuhakikisha usalama wa mji huo.

Syria imeeleza tishio la Marekani kwamba itashambulia kwa makombora kuwa ni “shinikizo la kivita lisilo na maana,” shirika la habari la serikali ya Syria limesema.

Umoja wa Mataifa na washirika wake kadhaa wameelekeza lawama kwa majeshi ya Syria kuwa yanahusika na mauaji hayo, wakati Syria na Urusi  wamekanusha kuwa majeshi ya Rais Bashar al-Assad yalihusika na shambulizi hilo la kemikali.

Waziri wa Ulinzi wa Marekani Jim Mattis amesema kuwa Marekani bado inafanya tathmini ya kintelijensia juu ya shambulizi hilo lililotokea Syria. “Tunakaa tayari kuchukua hatua za kijeshi mbalimbali iwapo zitakuwa zinaafikiana na maamuzi ya rais,” amesema Jumatano.
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

 
Support : Copyright © 2018. AFRICAN NEWS BLOG - All Rights Reserved
Imetengenezwa na Edwin Moshi
Inaendeshwa na AFRICAN NEWS BLOG