Home » » Shirika la Ndege nchini(ATCL) limeondolewa katika mfumo wa malipo wa Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga(IATA) kutokana na madeni

Shirika la Ndege nchini(ATCL) limeondolewa katika mfumo wa malipo wa Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga(IATA) kutokana na madeni

Unknown | Thursday, April 12, 2018 | 0 comments
Shirika la Ndege nchini ATCL limeondolewa katika mfumo wa malipo wa Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga IATA kutokana na kukabiliwa na madeni na sasa limetiliana saini ya makubaliano ya miaka mitano na Kampuni ya Ndege ya HAHN Air kuuza tiketi za Air Tanzania.

Akizungumza na wanahabari huko Zanzibar, Mkurugenzi wa ATCL Mhandisi Ladislaus Ernest Matindi, amesema wamelazimika kuingia kwenye makubalianao na kampuni hiyo ili wasikose baadhi ya huduma za malipo ya tiketi.

"Tuna madeni, sikumbuki yalifikia kiasi gani lakini ni madeni makubwa ambayo yalilazimisha kusimamishwa uanachama au kufungiwa huduma hizi mpaka tutakapokuwa tumelipa hayo madeni.

"Kubwa zaidi ilikuwa ni sisi kuwa katika mfumo wa shirikisho wa mashirika ya ndege dunia IATA ambayo ndo mfumo wa uuzaji na utawanyaji wa Tiketi. Maana mabadilishano ya pesa au kupeleka pesa kutoka shirika moja kwenda lingine hufanyika kwa kutumia huo mfumo wa IATA. Hii tunaanza kufanya ni kupitia kwakweli mgongoni kwa mtu.

"Hawa ni wanachama ambao wamepewa leseni ya kutoa huduma kwa mashirika ambayo hayapo kwenye mfumo wa IATA. Lazima tulipe madeni yetu tuliyonayo AITA ni mabilioni 'ni pesa nyingi kwa kweli' ili tuweze kurudi kwanza kwenye mfumo wa kukusanya pesa" Amesema Mhandisi Ladislaus Ernest Matindi. 

==>>Msikilize Hapo Chini
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

 
Support : Copyright © 2018. AFRICAN NEWS BLOG - All Rights Reserved
Imetengenezwa na Edwin Moshi
Inaendeshwa na AFRICAN NEWS BLOG