Mmiliki wa Shule ya Sekondary ya St. Patrick ya jijini Dar es Salaam, Ndele Mwaselela amejitolea kumsomesha mtoto wa marehemu Agnes Masogange, Sania(11) kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne na akifaulu hadi chuo kikuu.
Hii ni neema nyingine kwa mtoto huyo wa pekee wa Masogange aliyemuacha, baada ya jana kamati ya maandalizi ya mazishi kupitia mweka hazina wake, Zamaradi Mketema kueleza kuwa wamemwekea Sh2 milioni zilizobaki katika michango ya msiba huo kwenye akaunti yake.
Zamaradi amesema fedha hizo zimewekwa mahususi kwa ajili ya kumsaidia kianzio katika cha ada atakapoanza kidato cha kwanza mwakani kwa kuwa mwaka huu anatarajiwa kumaliza darasa la saba.
Akizungumza leo Jumatatu Aprili, 23 katika shughuli za mazishi, zilizofanyika nyumbani kwa baba wa Masogange, Kijiji cha Utengule, Wilaya ya Mbalizi, Mwalesela amesema mbali ya kumsomesha pia mtoto huyo atakaa hosteli kwa gharama zake kwa muda wote wa masomo yake.
“Akifaulu kidato cha nne pia atasomeshwa na mimi hadi kidato cha tano na sita lakini pia akifaulu atakwenda hadi chuo kikuu,” |amesema.
Kutokana na maamuzi hayo, alimtaka msanii Irene Uwoya ambaye mtoto wake naye anasoma katika shule hiyo, kuhakikisha anapokwenda kumsalimia mwanaye awe anakwenda kumsalimia na Sania.
“Hivyo wewe msanii Uwoya una mtoto wako pale shuleni kwangu naomba ukija kumuona hakikisha unamuona na mtoto huyo,” amesema Mwaselela
0 comments:
Post a Comment