Wanawake Wilayani Makete Mkoani Njombe wamesema Matukio ya Unyanyasaji na Mfumo Dume umepungua kwa kiasi kikubwa kufuatia Elimu ambayo imekuwa ikitolewa Mara kwa Mara kwa Wanaume.
Hayo yamejiri jana katika Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani ambayo katika Wilaya ya Makete yalifanyika Kata ya Iniho Tarafa ya Magoma Wilayani hapa.
Wanawake hao Katika Risala yao waliyoisoma Mbele ya Mgeni Rasmi Bi.Upendo Mgaya kwa Niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Makete Mh.Veronica Kessy,wamesema unyanyasaji na Mfume Dume uliokuwa ukitumika na wanaume kuwakandamiza Wanawake kwa sasa Matukio hayo yamepungua kwa kiasi kikubwa na kuwaomba Wanaume kuwawezesha Kiuchumi na kuwaunga mkono katika shughuli zinazofanywa na wanawake hao zikiwemo za Ujasiriamali.
Bi.Upendo Mgaya katika Hotuba yake kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya Mh.Veronica Kessy amewapongeza wanawake kwa Moyo wao wa Uvumilivu na Ujasiri wa kuweza kubeba majukumu ya Kifamilia,Kujihusisha na shughuli za Kilimo na Ujasiriamali.
Pia amewapongeza Wanaume wote waliofika siku hiyo katika Maadhimisho hayo huku akiongeza kuwa "uwapo wenu hapa ni Matumaini yangu kwamba mtakuwa Mabalozi wazuri katika kupeleka ujumbe wa Kaulimbiu wa Kuimarisha usawa wa Kijinsia na kuwawezesha Wanawake Vijijini ili waweze kushiriki katika shughuli za Kiuchumi''
"Sote kwa Pamoja tuchukue jukumu la kumsaidia Mwanawake ili aweze kushiriki vizuri katika mchakato wa kuelekea Uchumi wa Viwanda na Hatimaye Tanzania ya Viwanda" Aliongeza Bi.Upendo Mgaya.
Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Iniho ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Makete Mh.Jinson Mbalizi amewapongeza Wanawake hao kwa maadhimisho hayo pamoja na wanaume waliowaunga Mkono wanawake hao,huku akiahidi kwa niaba ya wanaume wenzake kuyashughulia matatizo ya wake zao kwa kuwasaidia Kimawazo,Kiuchumi na mambo mengine yanayohusu Familia.
Wakati huohuo Wanawake Watumishi wa Umma walnaofanya kazi Makao Makuu ya Halamashauri ya Wilaya ya Makete wametoa Msaada wa Vitu mbalimbali kama Chakula,Matunda,Sabuni,Sukari,Mafuta ya Kupikia,Mchele na vitu vingine kwa Wanawake wenye watoto wachanga waliopo Hospitali ya Wilaya Makete
Pia wamewakabidhi wanawake hao wenye watoto wachanga Kiasi cha fedha Laki moja kumi na tano Elfu(115,000) kwa ajili ya Mahitaji ya watoto wao
Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo Bi.Anamaria Kanyawana amewashukuru Akinamama hao kwa moyo wao wa Upendo kwa kutoa vitu hivyo kwa Wanawake hao
0 comments:
Post a Comment