Home » » WANANCHI WAKARABATI BARABARA KWA MIKONO NA MAJEMBE IVALALILA MAKETE-NJOMBE

WANANCHI WAKARABATI BARABARA KWA MIKONO NA MAJEMBE IVALALILA MAKETE-NJOMBE

Unknown | Monday, March 12, 2018 | 0 comments
 Gari dogo likipita lililotokea Mbeya na wananchi wakalisimamisha na kudai hela ya Mchango ili kusaidia kazi wanayoifanya
 Wananchi wakiendelea kumwaga mawe wanayochimba kwa mkono na Majembe
 Magari yakiwa yamekwama baada ya Gari kubwa la Tani 10 lililotangulia kuharibika katikati ya Barabara likiwa limebeba Mkaa

Gari la Kampuni ya Japanese likiwa Pembezeni Mwa Barabara baada ya kuteleza na kuegamia Ukuta
 Wananchi wakiendelea na shughuli ya kufyeka Miti kandokando mwa Barabara ya Ivalalila-Nkenja

 Wananchi wakikata miti iliyopo kandokando mwa Barabara kwa kutumia Mashine ya Chain

 Mabasi ya Abiria Kampuni ya Japanese yakinasuana baada ya Basi lingine kutoka Makete kukwama na Kusaidiwa kukwamuliwa na lile lililotokea Jijini Mbeya
 Scania kubwa iliyoharibika katikati ya Barabara kwa siku 5 zilizopita baada ya Kubeba Mkaa ikitokea kijiji cha Kisinga kata ya Lupalilo

Wananchi wa Kitongoji cha Ivalalila kilichopo Ndani ya Mamlaka ya Mji mdogo Iwawa Wilayani Makete Mkoani Njombe wameamua kujitokeza na kutengeneza Barabara kwenye maeneo korofi kutoka kijiji hapo mpaka kijiji jirani cha Nkenja kilichopo kata ya Kitulo kwa lengo la kupata huduma za usafiri wakati wote.

Wananchi hao wamesema wameamua kutengeneza Barabara hiyo ambayo ni ya Muhimu sana kwa Wananchi hao na Wananchi wengine wanaosafiri kutoka Ikonda,Makete na Vijiji vingine ikiwemo Ivalalila yenyewe kuelekea Jijini Mbeya.

Uamuzi huo umekuja baada ya kuona Barabara hivyo ambayo ipo chini ya Tanroad Mkoa wa Njombe inazidi kuharibika na kuleta usumbufu mkubwa kwa wasafiri kwa kutumia muda mwingi kukaa barabarani kwa sababu ya ubovu wa Barabara hiyo.

Mwakilishi wa TANROAD Wilayani Makete aliyepo Njombe Injinia Meta alipotafutwa na Kitulo Fm kuzungumzia hali ya Barabara hiyo na mpango wao wa kuhudumia Barabara zilizochini ya Tanroad Wilaya ya Makete amesema kwa sasa yuko sehemu isiyo nzuri hivyo hawezi kuzungumzia kwa undani zaidi suala hilo huku akiahidi kufika Makete mda wowote kwa ajili ya kushughulikia Tatizo hilo. 

"Kuna mahala nipo nafanya kazi na vibarua lakini nitalizungumzia hilo nikija" alisema baada ya kuulizwa na mwandishi wetu kwa njia ya simu.

Alipoulizwa Je ni lini sasa atafika Makete kushughulikia tatizo la Barabara kwenye maeneo korofi Aliongeza kwamba"Nafanya kazi nyingi lakini kwa sasa mvua nyingi mno ila  tutaongea nipo sehemu yenye watu wengi" Alimaliza Injinia Meta.
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

 
Support : Copyright © 2018. AFRICAN NEWS BLOG - All Rights Reserved
Imetengenezwa na Edwin Moshi
Inaendeshwa na AFRICAN NEWS BLOG