Mila potofu iliyojengeka miongoni mwa wananchi Wilayani Makete Mkoani Njombe ya kuwa Makete hakuna Ugonjwa wa Malaria jambo ambalo linapingwa vikali na wataalamu wa Masuala ya Afya .
Uchunguzi uliyofanywa na kitulo fm imebani kuwa wanachi wilayani makete hawatumii vyandarua kwa madai ya kwamba Makete hakuna Mbu wanaowexa kuambukiza ugonjwa wa ugonjwa wa maralia kutokana na hali ya hewa kuwa ya ubaridi sana.
Wakizungumza na kitulo fm wananchi hao wamesema hawaoni sababu ya kutumia vyandarua kwa ajili ya kujikinga na Mbu kwani wilaya ya makete hakuna mbu ambae anaambukiza ugonjwa huu na wao hawajawai kuugua ugonjwa huo.
Bwana LEONAD SANGA ni mkazi wa Makete makete yeye amesema anapingana na matumizi ya vyandarua wanavyoletewa na waisani na kusema kuwa vyandarua vinatakiwa kupelekwa kwenye maeneo ya joto na sio kwenye baridi kama wilaya ya makete .
Naye Bi.DELILA ASHELI SANGA amesema wananchi wana imani potofu kwa sababu Makete hakuna Magonjwa yanayotokana na Mbu na wakichukua Vyandarua wanatumia kwa matumizi tofauti kama kutengeneza kamba za kufungia kuni pamoja na kufunikia mabanda ya kuku na bustan za mbogamboga.
CRISTOPHA MUSIKA ni Mratibu wa Maralia wilaya ya makete ambapo amesema kumekuwa na imani potofu kutoka kwa baadhi ya wananchi kuhusu vyandarua kwamba vinapunguza nguvu za kiume jambo ambalo sio kweli kwani vyandarua hivyo vimewekwa dawa ambayo imethibitishwa haina madhara yeyote kwa binadamu.
Bw.MUSIKA amesema Takwimu zinaonyesha Ugonjwa wa malaria upo katika Wilaya ya Makete na kuna watu wanakufa kutokana na Ugonjwa huo.
Ameongeza kwamba kwa mwaka 2017 Wagonjwa waliofika na kupima na kuondoka kwenye Hospitali ya Wilaya wanawake na wanaume ni wagonjwa 720.
MRATIBU huyo amewataadharisha wananchi wanao chukua vyandarua na kuvitumia kwa matumizi ambayo siyo sahihi ikiwa ni pamoja na kuvikata na kuzungushia bustani pamoja na kutengenezea mabanda ya kuku amesema sheria zipo wazi na kwa sasa wamejipanga kwa yoyote atakae patika atachukuliwa hatua kali kwa mujibu wa Sheria na amewataka wanao tenda jambo hilo kuacha mara moja.
0 comments:
Post a Comment