Mwanamke mmoja Emmy Sanga Mkazi wa Kitongoji cha Dombwela Kijiji cha Iwawa Wilayani Makete Mkoani Njombe amemtundika mtoto wa Kiume mwenye miaka miwili juu ya Kabati na kufunga mlango kwa nje huku yeye akienda kuuza Baa eneo la Kona
Mtoto huyo amegundulika baada ya Timu ya Ulinzi na Usalama wa mtoto kupita eneo hilo na kugundua kuwa mtoto huyo analia na amefungiwa ndani akiwa juu ya Kabati pasina Msaada wowote kwa kuwa wakati huo hapakuwa na mtu nyumbani hapo wa kuweza kumsaidia
Mwanamke huyo alipotafutwa aligundulika kumuacha mtoto yeye akiwa ameelekea kufanya biashara ya kuuza Baa eneo la Konambali na nyumbani hapo,ndipo timu hiyo ya Ulinzi na Usalama ngazi ya Wilaya ilipowasiliana na Jeshi la Polisi lililofika Nyumbani hapo na kujionea hali halisi
Mwanamke huyo yupo Kituo cha Polisi Makete kwa ajili ya Mahojiano zaidi
Alipoulizwa na Mwandishi wetu Veronica Mtauka ambaye ni Mjumbe wa Kamati hiyo amesema''Mimi sijampandisha juu ya kabati huyu mtoto atakuwa amempandisha kaka yake,lakini ukweli mimi sijawahi kumfungia mtoto huku juu''
''Nilikuwa nimeenda kuuza baa kule kona lakini nilimwacha hapa kitandani sijui kapandaje huko juu'' aliongeza
Mtoto wake wa pili kati ya watoto watatu anayesoma Darasa la tatu shule ya Msingi Makete mwenye miaka(10) amesema yeye ndiye hushinda na mdogo wake mpaka usiku wakati wa kwenda kulala
Mwanamke huyo amekiri kurudi nyumbani saa nne usiku mara baada ya kazi na kukuta watoto wameshalala tayari bila kujali wamekula nini
Amesema Baba aliyezaa naye mtoto huyo yupo Makete Mjini na amemtelekeza kwa hiyo kila kila watoto wake analazimika kujitegemea yeye mwenyewe na kutafuta pesa kwa njia ya kuuza baa ili aweze kuwalea watoto wake
0 comments:
Post a Comment