Home » » MH.SUZAN KOLIMBA AKABIDHI VITABU 847 SHULE 6 ZA SEKONDARI MAKETE

MH.SUZAN KOLIMBA AKABIDHI VITABU 847 SHULE 6 ZA SEKONDARI MAKETE

Unknown | Monday, March 12, 2018 | 0 comments

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mh.Dr.Suzan Kolimba Katikati akiwa katika Picha ya Pamoja na Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana(Makete Girl's) iliyopo Kijiji cha Utweve Kata ya Ukwama

Wanafunzi shule ya Sekondari ya Wasichana Makete(Makete Girl's)wakiwa katika Picha huku wakiwa wameshika Vitabu walivyopewa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mh.Dr.Suzan Kolimba 


Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mh.Dr.Suzan Kolimba amekabidhi Vitabu 847 vya Masomo Mbalimbali kwa shule sita za Sekondari Wilayani Makete Mkoani Njombe.

Dr.Suzan Kolimba amekabidhi vitabu hivyo katika kupambana na upungufu wa Vitabu vya Kiada Ziada Shule za Sekondari zilizopo Wilayani Makete akiwa katika Ziara yake ya siku tatu Wilayani hapa.

Shule zilizonufaika na Vitabu hivyo ni Shule ya Sekondari ya Wasichana Makete(Makete Girl's) Vitabu 147,Shule ya Sekondari Usililo 120,Shule ya Sekondari Matamba 120,Shule ya Sekondari Kitulo 120,Shule ya Sekondari Mlondwe 120 na Mwakavuta Vitabu 120.

Akiwa katika Ziara hiyo Dr.Suzan amesema Elimu kwa Watoto ni Haki yao,Hivyo yeye kama Kiongozi na Mama Mzazi ndiyo maana anawajibika kuhakikisha Watoto wanapata Elimu bora katika Mazingira Mazuri yenye vitendea kazi vya kutosha.

Kwa Upande wa Wanafunzi kutoka shule zilizonufaika na Vitabu hivyo wamemshukuru Mh.Kolimba kwa Msaada huo na kumuahidi kufanya Vizuri katika Mitihani Mbalimbali.
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

 
Support : Copyright © 2018. AFRICAN NEWS BLOG - All Rights Reserved
Imetengenezwa na Edwin Moshi
Inaendeshwa na AFRICAN NEWS BLOG