Wabunge wamefika Gereza Kuu la Ruanda jijini Mbeya kumjulia hali mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi 'Sugu'.
Waliomtembelea Sugu ni mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema na wa Tandahimba (CUF), Katani Katani.
Sugu
na Katibu wa Chadema Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Emmanuel Masonga
wapo mahabusu wakikabiliwa na kesi ya kutumia lugha ya fedheha dhidi ya
Rais John Magufuli.
Lema
na Katani wakiongozwa na mwenyeji wao Mbunge wa Viti Maalumu, Sophia
Mwakagenda pia wamefika nyumbani kwa Desderia Mbilinyi, mama mzazi wa
Sugu eneo la Sae jijini Mbeya kwa ajili ya kumfariji na kumtia moyo
kutokana na misukosuko anayopitia mtoto wake.
Wakizungumza na familia ya Sugu, wabunge hao wamesema yupo gerezani kwa kuwa anapigania haki za wananchi.
Lema amemtaka mama huyo kuwa na moyo wa uvumilivu.
0 comments:
Post a Comment