Rais
Dkt. John Magufuli amesema mara zote anaposikia matatizo yametokea eneo
fulani fulani huwa anajiuliza akimbilie wapi ili aweze kupata msaada wa
utatuzi wa jambo hilo bila ya kuleta athari yeyote katika taifa.
Rais
Magufuli ametoa kauli hiyo leo (Jumapili Februari 04, 2018) wakati
alipohudhuria hafla ya kumweka wakfu na kumsimika Mchungaji Jackson
Sosthenes kuwa Askofu wa tano wa Kanisa la Anglikana Dayosis ya Dar es
Salaam.
"Sisi
viongozi wa serikali mara nyingi huwa tunawategemea viongozi wa
makanisa na misikiti katika kutuongoza, nafahamu serikali haina dini
lakini naheshimu sana dini na kuthamini mawaidha pamoja na mafundisho
yanatolewa na viongozi wa dini wawe waislamu, wakristo hata wahindu
tunayaheshimu sana", alisema Rais Magufuli.
Pamoja
na hayo, Rais Magufuli aliendelea kwa kusema "siku zote sisi viongozi
ndani ya serikali huwa tunafurahi sana kuona makanisa na misikiti ikiwa
imetulia, unaposikia mahali fulani fulani kuna migogoro sisi viongozi na
hasa mimi huwa najiuliza ninapopata matatizo ntakimbilia wapi. Kwa
sababu makanisa na misikiti ni sehemu ya uponyaji wa roho zetu. Uponyaji
wa roho ni mahali ambako kuna manufaa zaidi kuliko kwenye uponyaji wa
mwili".
Kwa
upande mwingine, Dkt. Magufuli amedai endapo mahali kwenye uponyaji wa
mwili ukisikia kumeanza matatizo basi unapaswa kutazambua jinsi taifa
unaloliongoza roho zake zitakavyopotea.
0 comments:
Post a Comment