Na Jumbe Ismailly, Singida
IDARA
ya Uhamiaji Mkoa wa Singida inawashikilia kwa uchunguzi watoto wa kike
watatu raia wa Rwanda wenye umri chini ya miaka 18 kwa tuhuma za
kuingia nchini kinyume cha sheria.
Kaimu
Ofisa Uhamiaji Mkoa wa Singida,Kamishna Msaidizi, Angela Shija amesema
watoto hao wenye umri kati ya miaka 9 na 13 walikamatwa Januanri
30,mwaka 2018 wilayani Manyoni.
Amesema walikuwa wakitokea nchini Rwanda wakielekea nchini Zambia kuwaona wazazi wao.
“Januari 30 mwaka 2018, ofisi ya Uhamiaji Mkoa wa Singida ilifanikiwa kuwakamata watoto wa kike watatu raia wa Rwanda.
“Walikamatwa
wilayani Manyoni mkoani Singida wakiwa kwenye basi namba T 265 BFY mali
ya Kampuni ya Katagi,” amefafanua Kamishina huyo msaidizi
Kwa
mujibu wa Ofisa Uhamiaji Idara ya Uhamiaji ilifanikiwa kuwakamata
watoto hao kutokana na taarifa za raia wema na watoto hao wamedai
wanaelekea nchini Zambia kuwaona wazazi wao.
Hata
hivyo Kamishina Msaidizi huyo wa Jeshi la Uhamiaji aliweka bayana kuwa
Idara ya Uhamiaji mkoani Singida inaendelea na uchunguzi ili kubaini
watu waliojihusisha na biashara hiyo ya usafirishaji wahamiaji haramu.
Aidha
Kaimu Ofisa Uhamiaji Mkoa wa Singida ametoa mwito kwa wananchi kujenga
utamaduni wa kutoa taarifa kwenye ofisi zao au kwenye vituo vya polisi
vilivyo karibu mara wanapowaona watu wasiowafahamu.
Amefafanua
kuwa taarifa hizo zitaisaidia Uhamiaji kufanyia kazi za kubaini
matukio ya watu wa aina hiyo na kuwachukulia hatua za kisheria.
Amesisitiza
baada ya uchunguzi kukamilika na kuwabaini waliohusika katika biashara
hiyo ya kuwasafirisha,na kwa sababu wana umri chini ya miaka 18,watoto
hao watarudishwa nyumbani kwa wazazi wao nchini Rwanda.
0 comments:
Post a Comment