Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Dkt. John
Pombe Magufuli, kesho tarehe 03 Februari, 2018 atawatunuku kamisheni
maafisa wapya wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) katika
viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Watakaotunukiwa
kamisheni ni maafisa wapya wa Tanzania na kutoka nchi marafiki
waliopata mafunzo katika Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi Monduli Mkoani
Arusha.
Tukio
la kutunuku kamisheni kwa maafisa hao litarushwa moja kwa moja na
vyombo vya habari vya redio, televisheni na tovuti rasmi ya Ikulu ambayo
ni www.ikulu.go.tz kuanzia saa 3:00 asubuhi.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
02 Februari, 2018
0 comments:
Post a Comment