Hivi
karibuni msanii wa nyimbo za Bongo fleva nchini, Naseeb Abdul maarufu
duniani kama Diamond Platinumz amekuwa akiingia katika skendo za
kuchepuka kimapenzi na baadhi ya mastaa mbalimbali hapa nchini akiwemo
Tunda na Wema Sepetu.
Kufuatia
matukio hayo mama watoto wa Diamond , Zarinah Hassan ameamua kuchukua
uamuzi mgumu alioufanya kwa vitendo zaidi kuliko maneno kama ambavyo
imezoeleka na kuacha maswali mengi kwa mashabiki wa wawili hao.
Wengi
walitegemea kuona Zari akimlushia vijembe baba watoto wake kama ambavyo
imekuwa kipindi cha nyuma Diamond alipopata skendo na Hamissa Mobeto.
Zari
kupitia akaunti yake ya instagram yenye wafuasi milion 3 na zaidi
ameamua kumu-unfollow baba watoto wake, Diamond Platinumz kitu ambacho
kimezua gumzo mtandaoni.
Ujumbe cha mwisho aliopost Zari kabla ya kuchukua uamuzi huo ulikuwa ni:
”There is no secret in life, whatever your Goals, you can get there if you are willing to work”, akimaanisha,
”Hakuna
siri katika maisha, unaweza kufikia malengo ikiwa una nia ya kuyafikia,
na kufikia malengo yako unatakiwa kuamua na kuwa tayari”. Alituma
post hiyo January 30, 2018, siku ambayo Diamond na Wema Sepetu wakiwa
stori kubwa ya siku baada ya kuonekana klabu pamoja.
Hayo
yamejiri siku chache zilizopita wakati wa uzinduzi wa kumtambulisha
rasmi Maromboso katika familia ya WCB, Wema Sepetu akiwa kama mgeni
mwalikwa katika shughuli hiyo.
0 comments:
Post a Comment