Anne
Kilango amesema kuwa ana uhakika kuwa jimbo hilo safari hii lazima
litarudi CCM na kudai kuwa yeye mwenyewe alhamisi anakwenda Siha
kuongeza nguvu na kuhakikisha ushindi unapatikana.
Mbunge
huyo kwa kujiamini kabisa akiwa Bungeni leo amewathibitishia Watanzania
kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kitashinda jimbo la Siha lakini
hakuzungumzia kabisa kuhusu jimbo la Kinondoni ambalo pia Februari 17
litafanya uchaguzi wa marudio ilihali chama chake hicho pia kinashiriki
katika uchaguzi huo, jambo ambalo linafanya watu waanze kujiuliza chama
hicho kimekata tamaa kushinda katika uchaguzi huo wa Kinondoni?
"Alhamisi
ya wiki hii mimi nahamia Siha na naomba Watanzania wawe na uhakika
kwamba Siha litakuwa jimbo la Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mhe. Naibu
Spika naomba nikuhakikishie kwamba CCM inashinda Siha" alisisitiza Anne Kilango Malecela
Mbali
na hilo Mbunge huyo aliiombea Wilaya hiyo ya Siha kwa Waziri wa Nishati
na Naibu Waziri ili iweze kupata umeme katika maeneo ambayo bado
hayajapata umeme ili yaweze kupata umeme kipindi hiki.
Wananchi
wa jimbo la Siha na Kinondoni wanategemea kufanya uchaguzi wa marudio
Februari 17, 2018 kuchagua wabunge ambao watawawakilisha kwenye Bunge la
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
0 comments:
Post a Comment