Mbunge
wa Kigoma Mjini (ACT- Wazalendo), Zitto Kabwe amesema amepatikana
mwekezaji wa kujenga maduka makubwa la biashara (malls) mkoani humo kama
yale ya Mlimani City ya jijini Dar es Salaam.
Akihutubia
mkutano wa hadhara katika viwanja vya Community Center, Mwanga jana
Januari 20, 2018, Zitto amesema haiwezekani mkoa wa Kigoma ukaendelea
kubaki nyuma kimaendeleo.
Zitto
ambaye pia ni Kiongozi wa ACT- Wazalendo amesema inapofika jioni mji wa
Kigoma unakuwa kimya jambo alilodai kuwa haliwezi kuleta mabadiliko na
kukuza mzunguko wa fedha.
“Tumepata
mwekezaji wa kujenga mall kubwa kama ya Mlimani City ili ikifika usiku
kuwe kumechangamka. Hatuwezi kuendelea kuwa mkoa au mji wa mwisho,”
amesema Zitto na kuongeza,
“Haina
maana sisi watoto wenu kusomeshwa na kuuacha mji huu ukaendelea kuwa
hivi. Tunahangaika, mtuache tufanye kazi na mwaka 2020 mtaniuliza
kupitia kile nilichoahidi na mtaninyonga kwa nilichowaahidi.”
Kuhusu
mapato ya halmashauri ya Kigoma Ujiji, Zitto amesema kitendo cha
Serikali kuu kuchukua vyanzo vya mapato vilivyokuwa vikiiingizia mapato
halmashauri hiyo na kutekeleza mipango yake, imewalazimu kuongeza kodi
kwa wafanyabishara.
“Tukiwaumiza
kidogo katika kodi tuvumiliane na mimi sitawaangusha lakini huwezi
kwenda peponi bila kufa, kwa hiyo lazima tuumie kidogo na nitakuwa
kiongozi mwongo nikija hapa na kusema kila kitu mtapata ni uongo,”
amesema Zitto na kuongeza,
“Sisi
hatuna wa kutubeba. Lazima tupambane wenyewe na tutiane moyo. Hakuna
jambo baya tunapopambana kuleta maendeleo lakini wengine wanaturudisha
nyuma, haipendezi, tutiane moyo jamani.”
Amesema lengo ni kuubadili mji wa Kigoma kwa kuwa umekuwa nyuma kwa muda mrefu.
0 comments:
Post a Comment