WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali itatuma wakaguzi ili wakague mali za Chama cha Ushirika cha mkoa wa Mara.
Amesema Serikali imeanza kufuatilia mali za vyama vya Ushirika nchini zikiwemo za chama cha Ushirika mkoa wa Mara.
Waziri Mkuu alitoa kauli hiyo jana (Jumapili, Januari 21, 2018) katika kikao cha majumuisho ya ziara yake ya kikazi mkoani Mara.
Alisema ukaguzi huo utakwenda sambamba na kufuatilia fedha wanazodai waliokuwa watumishi wa chama hicho.
“Kumekuwepo na matatizo makubwa ndani ya vyama vya ushirika kiasi cha kudumaza maendeleo ya wananchi.”
Pia Waziri Mkuu aliitaka mikoa yote ikomeshe matumizi ya vipimo visivyo rasmi kama butura na kangomba ili mkulima wapate tija.
“Vipimo hivyo ni vya kinyonyaji na vinamwibia mkulima na kuwanufaisha wafanyabiashara jambo ambalo si sahihi.”
Pia
Waziri Mkuu aliziagiza Halmashauri zipunguze watumishi walio kwenye
Makao Makuu ya Halmashauri na kuwapeleka maeneo ya vijijini ili
wakawahudumie wananchi.
Alisema
watumishi watakaobaki Makao makuu ya Halmashauri wanatakiwa nao waweke
utaratibu wa usafiri ili kwenda vijijini kutatua kero za wananchi.
Kwa
upande wa kilimo, aliagiza Maafisa Kilimo wote wapelekwe vijijini
kuwahudumia wananchi na watakaobakia Ofisini ni Mkuu wa Idara, Afisa
Bustani na Afisa Utafiti tu.
0 comments:
Post a Comment