WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amemuagiza Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara Bw.
Raphael Nyanda kutuma timu ya wakaguzi kwenda kufanya ukaguzi maalumu
katika ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Butiama.
Amesema
Halmashauri hiyo imekuwa na tabia ya kutumia fedha za miradi mbalimbali
ya maendeleo zinazotolewa na Serikali katika shughuli nyingine jambo
ambalo ni kinyume cha sheria.
Waziri
Mkuu alitoa agizo hilo jana (Januari 20, 2018) wakati akizungumza na
watumishi na madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Bitiama katika ukumbi
wa chuo Kikuu cha Kilimo cha Mwalimu Nyerere cha Mara.
Pia
Waziri Mkuu aliagiza kuchunguzwa kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya
wilaya ya Butiama Bw Solomon Ngiliule pamoja na Mweka Hazina wa
Halmashauri Bw. Masanja Sabuni na Ofisa Manunuzi wa Halmashauri hiyo
Bw. Robert Makendo.
Alisema
viongozi hao wanatakiwa wachunguzwe kutokana na matumizi yasiyoeleweka
ya fedha za miradi ya maendeleo zinazotolewa na Serikali zikiwemo sh.
milioni 12 walizotumia kuandaa profile ya Halmashauri hiyo.
Waziri
Mkuu alisema fedha zingine ni pamoja na sh. milioni 70 za elimu
maalumu, sh. milioni 288 za mradi wa maji Butiama ambazo zote
hazijulikani zimetumikaje. “Hatuwezi kuvumilia vitendo hivi fanyeni
uchunguzi na naomba taarifa yake mara mtakapokamilisha.
Katika
hatua nyingine, Waziri Mkuu aliiagiza Taasisi ya Kuzuzia na Kupambana
na Rushwa (TAKUKURU) mkoani Mara imkamate na kumuhoji Meneja wa Wakala
wa Majengo Tanzania (TBA) mkoani Mara, Mhandisi Peter Salim baada ya
kushindwa kutekeleza ujenzi wa mradi wa ofisi za Halmashauri ya wilaya
ya Butiama.
Waziri
Mkuu alisema kuwa Serikali ilitoa sh milioni 600 Aprili, 2017 kwa ajili
ya kuanza kwa ujenzi wa ofisi za Halmashauri ya wilaya hiyo lakini hadi
sasa wakala huo haujafanya kazi yoyote.
Katika
maelezo yake Mhandisi Salim alisema ujenzi wa ofisi hiyo hadi
kukamilika utagharimu sh. bilioni tatu, kati ya sh. milioni 600
zilizotolewa na Serikali sh milioni 400 zimetumika kujengea msingi,
kauli ambayo ilipingwa na Mkuu wa wilaya hiyo Bibi Anna-Rose Nyamubi.
“Mheshimiwa
Waziri Mkuu siyo kweli kwamba kuna kazi inayoendelea bali kilichopo
pale ni mashimo ambayo hayajulikani ni ya nini. Pia kuna jengo moja
lilijengwa kwa mabati kama stoo na hakuna mafundi wanaoendelea na kazi”
Waziri
Mkuu alisema kuwa Serikali iko katika mchakato wa kuboresha mazingira
ya wafanyakazi ikiwa ni pamoja na ujenzi wa ofisi za watumishi na kwamba
haitamvumilia mtu yeyote atayekwamisha juhudi hizo.
Waziri
Mkuu baada ya kuwasili wilayani Butiama akiambatana na mkewe Mama Mary
Majaliwa walizuru kaburi la Baba wa Taifa marehemu Mwalimu Julius
Nyerere, katika Kijiji cha Mwitongo na kufanya mazungumzo na mjane wa
Baba wa Taia, Mama Maria Nyerere.
Baada
ya kuwasili katika eneo alilozikwa Mwalimu Nyerere, Waziri Mkuu na
Mkewe waliweka shada la maua juu ya kaburi na kisha walishirikiana na
wananchi kufanya maombi yaliyoongozwa na Chifu wa Wazanaki, Japheth
Wanzagi.
Pia
Waziri Mkuu alihutubia wakazi wa wilaya ya Butiama kwenye mkutano wa
hadhara uliofanyika katika uwanja wa Mwenge, ambapo alitumia fursa hiyo
kueleza juhudi mbalimbali za kuwaletea maendeleo zinazofanywa na
Serikali ya Awamu ya Tano, inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU
0 comments:
Post a Comment