Katibu
wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Itikadi
na Uenezi, Humphrey Polepole, amesema kama chama hicho kitajipanga
vizuri zaidi na kutekeleza majukumu yake kama inavyotakiwa, hakutakuwa
na upinzani.
Polepole
aliyasema hayo juzi, wakati akiwapokea viongozi kadhaa waliovihama
vyama vyao na kujiunga na CCM wakitokea mikoa ya Dodoma, Siginda, Tabora
na Kilimanjaro.
"Mimi
nawaeleza kama wana CCM tutajipanga vizuri na kuachana na ubinafsi,
heshima ya chama chetu mkoani Kilimanjaro itarejea kwa sababu
tutakapotekeleza majukumu yetu inavyotakiwa, upinzani hautakuwapo,"
alisema.
Viongozi
hao 37 kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na
ACT-Wazalendo walijiunga na CCM na kupokewa na Polepole katika ofisi za
chama hicho Mkoa wa Kilimanjaro mjini hapa.
Kwa
mujibu wa Polepole, chanzo cha kuhama kwa baadhi ya wanachama wa CCM
mwaka 2015 na kwenda upinzani, kilikuwa ukiukwaji wa misingi ya haki na
wajibu ndani ya chama hicho.
"Msingi
ya kuanzishwa kwa CCM ni kusimamia haki na wajibu wa watu, hivyo kuhama
kwa wanachama hao kulitokana na kukosekana kwa haki na CCM kukosa mvuto
kwa watu. Lakini sasa tumetambua ni wapi tumekosea ndiyo maana CCM ya
sasa imekuwa na mvuto,” alisema.
Aliongeza kuwa: "Kwasasa walioihama CCM wameanza kurejea Kutokana na chama sasa kurejesha imani, haki na wajibu kwa wanachama.”
Alisema
CCM ya sasa imejenga imani kubwa kwa Watanzania kutokana na kufanyika
kwa uboreshaji na utendaji kazi wa Mwenyekiti waTaifa CCM, Rais Dk. John
Magufuli.
Polepole
alisisitiza kwamba mageuzi makubwa yanayofanyika kwa sasa ndani ya
chama hicho yamerudisha chama mikononi mwa wananchi na kuwataka wana CCM
wasiwakatae wanachama wanaotoka upinzani.
Pia
aliwataka viongozi wa chama mkoani Kilimanjaro kuhakikisha
wanawasimamia watendaji wa serikali kwa karibu ili kuhakikisha
wanatimiza majukumu yao kwa mujibu wa sheria ikiwamo kutoa fedha za
mikopo kwa vikundi vya wanawake na vijana.
0 comments:
Post a Comment