WANAUME
wawili waliotuhumiwa kushiriki uchawi katika kaunti ndogo ya
Igambang’ombe, kaunti ya Tharaka-Nithi kenya, Jumatano waliuawa kwa
kupigwa mawe na umati wenye ghadhabu
Wawili
hao, wenye umri wa miaka 55 na 60, walifurushwa kutoka nyumbani na
kupelekwa katika soko la Kajuki ambapo waliuawa hadharani.
OCPD
wa Chuka Igambang’ombe Bw Barasa Sayia aliambia vyombo vya habari kuwa,
maafisa wa polisi waliarifiwa kuhusu kisa hicho lakini walipofika
katika soko hilo, wanaume hao walikuwa washafariki kutokana na majeraha
mabaya mwilini.
Mkuu huyo wa polisi alisema polisi wameanzisha uchunguzi kuhusu kisa hicho ili kubaini wanakijiji waliohusika.
Bw
Sayia aliwaonya wakazi dhidi ya kuchukua sheria mikononi mwao na
kuwaomba kupiga ripoti kuhusu washukiwa kwa polisi ili sheria ifuate
mkondo wake.
“Tumeanzisha uchunguzi wa kina ili kuwatia nguvuni na kuwashtaki wakazi waliohusika katika mauaji haya,” akasema Bw Sayia.
Wakazi
waliohojiwa na Taifa Leo lakini wakaomba wasitajwe majina, walisema
wanaume hao wawili wamekuwa wakiendesha shughuli za uchawi katika kijiji
hicho kwa muda mrefu sana na walikuwa washukiwa wakuu wa vifo vingi
ambavyo vimekuwa vikishuhudiwa eneo hilo, hasa vya watoto.
“Wanakijiji
walikuwa wamechoshwa na wazee hao kwa vitendo vyao dhalimu,” akasema
mmoja wa mwanakijiji. Miili ya wawili hao ilipelekwa katika mochari ya
Hospitali ya Chuka kwa upasuaji.
0 comments:
Post a Comment