Rais wa Tanzania John Magufuli
amekutana na wanamuziki wawili aliowasamehe takriban wiki tatu
zilizoita, licha ya kuwa walikuwa wanatumikia kifungo cha maisha jela
kwa kuwabaka wasichana 10 wa shule mwaka 2003.
Nguza Viking,
anayefahamika pia kama Babu Seya, na mtoto wake Johnson Nguza, ambaye
pia anafahamika kama Papii Kocha, walimshukuru Rais Magufuli kwa
kuwasamehe ambapo walimwimbia wakati walimtembelea katika Ikulu.
Gazeti
la Citizen lilimnukuu Magufuli akisema, "msinishukuru mimi, bali
mshukuru Mungu ambaye ndiye pekee aliye na nguvu za kusamehe".
Watetesi wa haki za watoto walikosoa msamaha huo.
Walikuwa wametumikia kifungo cha miaka 13 wakati waliachiliwa kwa kuwabaka wasichana walio kati ya umri wa miaka 6 na 8.
Wawili hao walikuwa miongoni mwa wafungwa 61 waliopata msamaha wa rais wakati wa hotuba yake ya uhuru.
0 comments:
Post a Comment