Wazazi
na walezi ambao hawatawapeleka watoto shule za Sekondari kukiona cha Moto
Kijiji cha Ihanga kata ya Ukwama Wilayani Makete Mkoani Njombe
M/kiti
wa Kijiji cha Ihanga Fedenicko Ndelwa amesema hayo akizungumza na Kitulo Radio
Fm mapema wiki hii ambapo amewataka wazazi kuwapeleka watoto shule
waliochaguliwa kujiunga na Masomo ya Sekondari
Amesema
hatua za kisheria zitafuatwa kwa mzazi au Mlezi ambaye hatatimiza wajibu wake
wa kumpeleka motto shuleni
‘‘Nitamke
wazi suala la wazazi au walezi ambao watashidwa kuwapeleka watoto wao shuleni
mwezi huu January,hawa nitawasimamia kidete mpaka nahakikisha wanafunzi
wanapelekwa shule’’
‘‘Halmashauri
ya kijiji hiki cha Ihanga ilikaa wiki iliyopita na ikajadili kwamba kila mtoto
ambaye anakuta amefaulu lazima mzazi awajibike kumpeleka Mwanaye shule kwa kuwa
mzazi hilo ni jukumu lake la kisheria,hivyo sisi tutafuata sheria’’
‘‘Kijiji
change kina Jumla ya Vitongoji vitano na Kila Kitongoji kwenye Mtaa wake
anaidadi ya wanafunzi waliofaulu kwenda Sekondari hivyo wanahakikisha
mzazi/Mlezi anapeleka Mwanaye shule’’
Kwa
upande wake Afisa Elimu Sekondari Wilaya ya Makete Mwalimu Jackob Meena amesema
suala la Elimu ni muhimu kwa watoto bila kubagua Jinsia,hivyo wazazi watambue
jukumu la kuwasomesha watoto ni lao
Pia
amesema wazazi wanatakiwa kuwa karibu sana na watoto wao wa kike kwa kuwasaidia
mahitaji muhimu ili wasirubuniwe na wavulana na kuwasababishia kushindwa
kuendelea na Masomo
‘‘Nilitaka
nikazie kwa watoto wa kike na wakiume Elimu ndio inaweza kuwasaidia katika
kujikomboa na Mazingira Magumu yanayowakabili’’
‘‘Katika
Elimu tunamambo matatu makuu ambayo tunapambana nayo ikiwemo Ujinga,Maradhi na
Umaskini sasa bila Elimu kupambana na hivyo vitu vitatu haiwezekani itakuwa ni
kazi ngumu sana’’
‘‘Hivyo
Wazazi na walezi naomba Muhakikishe watoto hawa wanapelekwa shule kwa kutambua
umuhimu huo wa Elimu’’
0 comments:
Post a Comment