Taarifa
kutoka Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zinaeleza kuwa Vikao
vya Kamati za Bunge vinatarajiwa kuanza Jumatatu tarehe 15 hadi 27
January, 2018 Mjini Dodoma, hii ikiwa ni kabla ya kuanza kwa Mkutano wa
Kumi wa Bunge.
Shughuli ambazo zimepangwa kutekelezwa katika kipindi cha vikao hivi ni pamoja na ziara za ufuatiliaji, uchambuzi wa miswada mbalimbali na kupokea maoni ya wadau, na kupokea taarifa za utendaji za wizara.
Kamati
tatu za kisekta ambazo zitakuwa na jukumu la uchambuzi wa miswada ya
sheria mbalimbali ni pamoja na kamati ya Katiba na Sheria, kamati ya
Ardhi, Maliasili na Utalii pamoja na kamati ya Huduma na Maendeleo ya
Jamii.
0 comments:
Post a Comment