Katika
hali isiyokuwa ya kawaida, mama mmoja mjamzito aliyefahamika kwa jina
la Vera Paschal (29), mkazi wa Kishiri, jijini Mwanza ameibua utata
baada ya kudaiwa amejifungua kopo.
Taarifa
za awali zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii zilidai kuwa, mama
huyo alifika kwenye Kituo cha Afya cha Igoma (pichani), akaomba
ajifungue kopo kitendo ambacho kiliwashtua wauguzi waliokuwa zamu siku
hiyo
“Wauguzi
walishangaa kweli, sasa mtu anasemaje anataka kujifungua kopo?
Tulishindwa kuelewa kwamba ana akili timamu au vipi lakini kwa jinsi
alivyokuwa akizungumza tulibaini anazo akili timamu,” alieleza mdau
mmoja mtandaoni aliyedai alishuhudia tukio hilo.
Hata
hivyo, vyanzo vingine vilidai kuwa, mama huyo alikuwa na ugomvi na
mumewe hivyo alifanya vituko vya kujifanya ana mimba akaficha kopo hilo
karibu na sehemu za siri ili kumuonesha mumewe kuwa anataka kutoa mimba
hiyo.
“Watu
bwana, kuna wanaosema eti alikuwa ana ugomvi na mumewe. Sasa sijui
katika kufanyafanya vituko, akaweka kopo sehemu za siri na kujifanya
kama anataka kujifungua,” kilidai chanzo.
Kutokana
na utata huo, Risasi Jumamosi lilifanya jitihada za kuzungumza na
mganga aliyekuwepo zamu katika Kituo cha Afya Igoma, Zaituni Mkurunge
ambapo alikanusha taarifa zilizokuwa zimesambaa kwenye mitandao ya
kijamii.
“Taarifa
zilizosambaa katika mitandao ya kijamii zikieleza kuwa kuna mama
amejifungua kopo katika kituo chetu si za kweli, bali Jumatano
(iliyopita) mchana majira ya saa 9:00 alasiri alikuja mama mmoja
mjamzito akiwa amepakiwa kwenye Bajaj akilalamika kuwa anataka
kujifungua kopo. “Lakini tulipompokea na kumpeleka katika chumba cha
wazazi tulimpima na tukagundua kuwa alikuwa na ujauzito wa miezi sita na
tulipomchunguza vizuri kweli tulikuta kopo la mafuta ya kujipaka lenye
ukubwa wa gramu 100 limeingizwa kwenye uke wa mama huyo.
“Ikabidi
tutumie utaalamu wetu kulitoa lile kopo ambapo tulichukua kama saa moja
hivi na tukafanikiwa kulitoa, tulimuuliza hili kopo nani amekuingizia,
alitujibu kuwa aliota usiku anaingiziwa kopo kwenye uke wake,” alisema
muuguzi huyo. Akizidi kusimulia tukio hilo, muuguzi huyo alisema
hawajawahi kukutana na tukio la namna hiyo ambalo wengine walilihusisha
na mambo ya kishirikina.
“Tukio
hilo lilitushangaza, sisi kama wauguzi hatuamini vitu vya kishirikina
lakini mimba yake ipo na ule mlango wa uzazi ulikuwa bado haujafunguka.
“Baada ya kumtoa lile kopo, tuliwaita polisi ili kufanya uchunguzi zaidi
kuhusu tukio hilo lakini wito wangu kwa wakina mama wajawazito wasiwe
na tabia ya kudanganya, wawe wanasema ukweli,” alisema muuguzi huyo. Kwa
upande wake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Naibu Kamishna wa Polisi,
Ahmed Msangi alithibitisha kutokea kwa tukio hilo. “Tukio hilo lipo
mikononi mwetu na uchunguzi unaendelea na itakapobainika kuwa mama huyo
ana kesi ya kujibu, hatua za kisheria zitachukuliwa,” alisema
Chanzo: Risasi Jumamosi
0 comments:
Post a Comment