Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
imetangaza siku mbili za maombolezo kati ya Jumatatu na Jumanne wiki
ijayo, kuwakumbuka watu 44 waliopoteza maisha katika mafuriko makubwa
yaliyotokea wiki hii jijini Kinshasa.
Mbali na mauaji hayo, makaazi ya
watu 5,000 yamejaa maji, huku makaazi mengine 192 yakiharibika ikiwa ni
pamoja na kuvunjika kwa madaraja na barabara.
Maeneo yaliyoathiriwa zaidi na mafuriko hayo ni pamoja na Ngaliema, Bandalungwa, Barumbu, Limete na Selembao.
Jiji la Kinshasa limeendelea kukabiliwa na mafuriko mara kwa mara
mvua inaponyesha kutokana na miundo mbinu mibaya hasa mitaro ya
kupitisha maji na msongamano wa makaazi ya watu.
Maakazi mengi ya watu yamejengwa katika maeneo ya milima, katika eneo hilo lenye watu Milioni 10.
0 comments:
Post a Comment