Home » » Waumini wa dhehebu la Coptic nchini Misri washerehekea Krismasi kwa hofu

Waumini wa dhehebu la Coptic nchini Misri washerehekea Krismasi kwa hofu

Unknown | Sunday, January 07, 2018 | 0 comments


Rais wa Misri Abdel Fattah el-Sissi akisalimiana na wafuasi wa dhehebu la Coptic wakati wa mkesha wa Krismasi Januri 06 2018AFP PHOTO / KHALED DESOUKI
Wakiristo wa dhehebu la Coptic nchini Misri wanasherehekea sikukuu ya krismasi hivi leo chini ya ulinzi mkali.
Usalama umeimarishwa nje ya Makanisa ya dhehebu hilo jijini Cairo na miji mingine kwa hofu ya mashambulizi ya kigaidi.
Jumamosi usiku, mkesha wa kuamkia siku ya Krismasi, rais Abdel Fattah al Sisi alikuwa miongoni mwa viongozi wa juu wa serikali ya Misri waliohudhuria mkesha sikukuuu hiyo katika Kanisa kuu la Coptic jijiji Cairo.
Akiwa na Kiongozi wa Kanisa hilo Papa Tawadros II , wafuasi wa dhehebu hilo walimshangilia rais Al Sisi na kumwambia kuwa wanampenda.
Wauamini wa Kanisa la Coptic wameendelea kuwa hatarini, tangu mwaka 2013 baada ya serikali kulipiga marufuku kundi la Muslim Brotherhood.
Wapiganaji wa Muslim Brotherhood na wale wa Islamic State wamekuwa wakilaumiwa kwa kutekeleza mashambulizi ya kigaidi dhidi ya Wakiristo ambao ni wachache nchini humo.
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

 
Support : Copyright © 2018. AFRICAN NEWS BLOG - All Rights Reserved
Imetengenezwa na Edwin Moshi
Inaendeshwa na AFRICAN NEWS BLOG