NA. DOKTA MUNGWA KABILI. ….0744 000 473.
Katika maeneo mengi ya vijijini ni jambo la kawaida sana kwa watu kuamka na kujikuta wakiwa wamechanjwa chale sehemu mbalimbali mwilini na wasijue chale hizo wamechanjwa na nani na kwa sababu gani.
Jambo hili halitokei maeneo ya vijijini tu bali hutokea na mijini pia.
Watu huamka asubuhi na kujipata wakiwa wamechanjwa chale bila kujua ni nani aliehusika na kuwachanja chale hizo na alifanya hivyo kwa sababu gani.
Katika makala ya leo tutapata kuwafahamu ni akina nani haswa wanao wachanja watu chale usiku wakiwa wamelala na huwa wanafanya hivyo kwa sababu gani.
Kwanini wachawi huwachanja watu chale usiku ?
Wachawi huwachanja watu chale kwa sababu mbalimbali. Baadhi ya sababu hizo ni kama ifuatavyo :
1. KUSOMA NYOTA ZA WAHUSIKA : Story ya maisha ya kila mtu huwa imeandikwa kwenye damu yake .
Kwa kutumia maarifa ya juu kabisa ya kichawi, wachawi wanaweza kusoma story nzima ya maisha ya mtu kwa kutumia damu yake.
Kwa lugha nyepesi ni kwamba katika ulimwengu wa rohoni damu ya mtu ni kama ubao ama kitabu ambacho kimeandiwa story nzima ya maisha ya mtu huyo.
Siri na mipango yote ya maisha ya mwanadamu ambayo amepangiwa na Mwenyezi Mungu imeandikwa katika damu yake.
Wachawi wakitaka kujua kuhusu siri hii huhaha kutafuta damu ya mtu ambae wanataka kujua kuhusu maisha yake.
Hivyo basi wachawi wanavyo mchanja mtu chale, pamoja na mambo mengine, hufanya hivyo kwa lengo la kupata damu ambayo wataitumia kusoma nyota ya mhusika.
KAMA AMBAVYO WATAALAMU WA KISAYANSI WANAWEZA KUJUA MAISHA YA MTU YAKOJE KWA KUMFANYIA MTU HUYO KIPIMO KIITWACHO FULL BLOOD PICTURE, BASI VIVYO HIVYO WACHAWI WANAWEZA KUJUA SIRI YA MAISHA YA MTU KWA KUTUMIA DAMU YAKE.
NAOMBA NIELEWEKE VIZURI KUHUSU KIPIMO CHA FULL BLOOD PICTURE NA KUJUA MAISHA YA MTU.
SIMAANISHI KWAMBA KWA KUMFANYIA MTU FULL BLOOD PICTURE MADKATARI WANAWEZA KUJUA MAISHA YA MTU HUYO YATAKUWAJE HAPO MBELENI LA HASHA.
NINA MAANISHA HIVI, KIPIMO CHA FULL BLOOD PICTURE NI KIPIMO KINACHO ONYESHA HALI HALISI YA AFYA YA MWANADAMU NA KAMA TUJUAVYO MAISHA NI AFYA NA AFYA NDIO MAISHA.
KWA KUFANYA FULL BLOOD PICTURE MADAKTARI WANAWEZA KUBAINI KAMA MHUSIKA ANA VIRUSI VYA UKIMWI, KISUKARI, PRESHA,SHINIKIZO LA DAMU, LEHEMU MWILINI NAKADHALIKA.
WANAWEZA KUJUA KAMA MTU NI MGONJWA AU ANA AFYA NJEMA.
NA KWA KUJUA KAMA MTU NI MZIMA BUKHERI WA AFYA AU ANASUMBULIWA NA MARADHI MAZITO NDANI YA MWILI WAKE NI SAWA NA KUJUA KUHUSU MAISHA YAKE KWA SABABU MAISHA YA MTU NI AFYA NA AFYA NDIO MAISHA YA MTU. UKIACHILIA MIPANGO YA MUNGU NA SHARI ZA WACHAWI, AFYA YA MTU NDIO INAYO AMUA UMRI WA MTU KUISHI. UHAI WA MTU UPO KWENYE DAMU YAKE.
Vivyo hivyo basi wachawi wanapo taka kujua siri za maisha ya mtu hufanya hivyo kwa kutumia damu yake. Hii ni kwa sababu maisha ya kila mwanadamu yameandikwa kwenye damu yake. Siri zote kuhusu maisha ya kila mtu zimefichwa kwenye damu yake.
2. KUIBA NYOTA : Hii ni sababu nyingine kwanini wachawi huwachanja watu usiku wakiwa wamelala. Hufanya hivyo kwa lengo la kuiba nyota zao. Suala la kuiba nyota huja baada ya kusoma nyota ya mhusika kupitia damu yake na kuona inafaa kuchukuliwa kwa matumizi mbalimbali kama vile biashara, mali nakadhalika.
3. KUPIMA KINGA YA MTU : Kama nilivyo eleza hapo juu kuwa ndani ya damu ya mtu ndimo kumefichwa kila kitu kuhusu mtu huyo.
Kila siri inayo muhusu mwanadamu, imeandikwa ndani ya damu yake .
Wachawi wanapo taka kupima mtu fulani ana kinga kubwa kiasi gani hufanya hivyo kwa kusoma damu yake au vitu vya mtu huyo ambavyo vimetokana na msukumo wa damu kama vile manii n.k.
Kumbuka kuwa kinga yoyote ile ya mtu huwa inakaa kwenye damu yake. Dawa anazo chanjwa mtu kwa ajili ya kinga, dawa anazo kula ama kunywa mtu kwa ajili ya kinga huwa zinaenda kukaa kwenye damu yake.
Sasa basi katika uchawi njia ya juu kabisa ya kujua kinga ya mtu ikoje ni kusoma damu yake.
Hivyo basi wachawi wanapo mchanja mtu chale, pamoja na mambo mengine, hufanya hivyo kwa lengo la kupima kinga ya mtu huyo..
Na lengo la kutaka kujua kinga ya mtu ni kujua mtu huyo kinga yake ina nguvu kiasi gani na wakisha jua nguvu ya kinga ya mtu huyo kitakacho fuatia baada ya hapo ni kutuma uchawi wa kuteketeza kwanza kinga kisha ili wapate urahisi au mwanya wa kutupa uchawi wao kwa mtu waliemkusudia.
4. KUPANDA MAPANDO YA KICHAWI : Inaeleweka vyema kwa wengi kuwa mwanadamu aliumbwa kwa udongo.
Wachawi wana amini sana katika jambo hili. Wao hawaishii tu kuamini kuwa mwanadamu aliumbwa kwa udongo bali wanaenda mbele zaidi na kumtreat mwanadamu kama udongo kabisa.
Na katika kudhihirisha hilo kwa vitendo, wachawi wanaweza kuutumia mwili wa mwanadamu kupanda mapando yao mbalimbali. Wachawi wanaweza kuutumia mwili wa mwanadamu ( ambao ni udongo) kama shamba la kupanda mapando yao.
Mapando yao yanaweza kuwa kwa faida yao wao kama wachawi huku mtu huyo wakimtumia kama shamba tu au yanaweza kuwa kwa ajili ya mtu huyo ili baadae aje ayavune katika maisha yake halisi.
Ndani ya mwili wa mwanadamu inaweza kupandwa roho ya mauti ambayo itakuwa inakua kadri mwanadamu anavyo kuwa na anaweza “ kula matunda” ya roho hiyo hata baada ya miaka ishirini. Inaweza kupandwa roho ya kukataliwa, roho ya umasikini, ufukara nakadhalika.
Kwa hiyo chale hizo zaweza kuwa ishara kwamba wachawi walikuwa wanalima kwenye mwili wako na kupanda mapando yao ya kichawi kupitia damu yao.
5. KUFUGIA MAJINI WACHAFU : Wachawi wanaweza kuutumia mwili wa mtu kama banda la kufugia majini wachafu ambao watakuwa wanawachukuwa kuwatumia kila watakapo wahitaji.,Majini hao wachafu wanaweza kukaribishwa kwenye mwili wa mtu kupitia chale hizo za kichawi. Chale hizo hutumika kama Antenna za kuwavuta majini wachafu ndani ya mwili wa mtu walie mkusudia.
6. KUMPAKA MTU NUKSI NA MIKOSI: Kama nilivyo sema hapo awali kuwa story ya maisha ya kila mtu huwa imeandikwa kwenye damu yake.
Kuna kanuni moja kubwa sana katika ulimwengu wa rohoni ambayo inasema chochote utakacho kiunganisha na damu ya mtu basi kinamezwa na kuwa sehemu ya damu ya mtu huyo na kitu hicho kikisha kuwa sehemu ya damu ya maisha ya mtu huyo basi kinakuwa sehemu ya maisha ya mtu huyo na kikisha kuwa sehemu ya maisha ya mtu huyo basi kitaanza kujidhihirisha chenyewe katika maisha ya mtu huyo.
Hii ni kwa sababu damu ndio nishati inayo endesha maisha ya mtu. Nishati hii ndio inayo amua kila kitu katika maisha ya mwanadamu.
Wachawi kwa kulitambua hilo, huwa wanafanya uchawi maalumu wa kuunganisha damu ya mtu na vitu vibaya ili vitu hivyo vibaya na vichafu vikafanyike kuwa sehemu ya damu ya mtu huyo na hivyo kuharibu utaratibu mzima wa maisha ya mtu huyo.
Hufanya hivyo kwa kuwatia watu nuksi.Nuksi hiyo inaweza kuingizwa kwenye mfumo wa maisha ya mtu kwa njia nyingi sana, kubwa kuliko zote ni njia hiyo ya kuwachanja chale na kuwapaka nuksi.
Nuksi sio neo tu kama baadhi ya watu wanavyo lichukuliwa. Sio neno wala msemo.
Ni uchawi kabisa ambao nguvu yake hubeba maudhui ya jina lake. Zipo nuksi za aina nyingi sana.
Moja wapo kati ya nuksi hizo ni nuksi inayo tengenezwa kwa vitu mbalimbali kama vile : Mavi ya mtu fresh ambayo alijisaidia akiwa porini, mavi ya nyani, mavi ya sokwe, mavi ya chatu, mavi ya kenge, uchafu wa kwenye majalala saba ( Wakati uchafu huu unachukuliwa hufanyika tambiko maalumu la kichawi linalo husisha kafara ya mnyama au ndege, ambayo hulenga katika kuwaamsha majini wachafu walio lala katika majalala hayo kuingia ndani ya uchafu huo), kipande cha mti kilicho okotwa ndani ya kaburi wakati kaburi linachimbwa, utumbo wa kuku, maji yaliyo tumika kuoshea maiti, uchafu wa mochwari, shahidi la kaburi, dawa moja ya kiarabu ifananayo na lami na yenye kutoa harufu mbaya sana , uchafu wa chooni pamoja na madawa mengine ya kichawi ambayo ninayahifadhi hapa)
Vitu vyote hivyo vinapikwa kwa pamoja kwa kutumia dawa ya paka mweusi.
Vinakaangwa hadi kuwa majivu halafu mhusika anaenda kupakwa kichawi usiku.
Wakati mwingine zoezi la kumpaka mtu nuksi huweza kuendana na zoezi la kumpaka damu mbichi ya mnyama mmoja apendwae sana na wachawi…
Damu hii hunuizwa kutamka mambo yatakayo enda kubatilisha mambo yote mazuri yaliyo andikwa kwenye damu ya mhusika.
Damu ya mnyama huyu huenda kufuta kila kitu kizuri kilicho andikwa kwenye damu ya mtu aliekusudiwa na badala yake yenyewe ndio hukaa na kuweka tamko jipya juu ya maisha ya mtu aliekusudiwa.
Matokeo yake mtu huyo huanza kuandamwa na nuksi mabalaa na mikosi .
Makala haya yameandaliwa na Dokta. Mungwa Kabili ambae anapatikana kwa SIMU NAMBA : 0744 000 473.
2 comments:
Wewe mbabaifu
Stori tu hapo
Post a Comment