MWENDESHA
Mashtaka Mwandamizi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana Rushwa
,(Takukuru) , Leonard Swai ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu
kuwa Rais wa Klabu ya Simba, Evans Aveva amelazwa Hospital ya Taifa ya
Muhimbili akisumbuliwa na Figo.
Aveva
ni mshtakiwa wa kwanza katika kesi ya uhujumu uchumi ambapo anashtakiwa
pamoja na Makamu rais wa klabu ya Simba, Godfrey Nyange ‘Kaburu’ ambaye
alikuwepo mahakamani hapo
Wakili Swai amedai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Victoria Nongwa kuwa upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika.
Amedai,
walishachukua maelezo ya mshtakiwa wa pili na kwamba wanaangalia jinsi
ya kupata maelezo ya mshtakiwa wa kwanza ambaye kwa sasa ni
mgonjwa.Baada ya kueleza hayo Hakimu Nongwa ameaihirisha kesi hiyo hadi
February 8,2018 kwaajili ya kutajwa.
Aveva
na Kaburu wanakabiliwa na mashtaka matano ya kughushi, kuwasilisha
nyaraka ya uongo na kutakatisha fedha Dola za kimarekani 300,000.
0 comments:
Post a Comment