Tajiri
na Mfanyabiashara mkubwa duniani, Bill Gates amemuonya rais wa Marekani
Donald Trump kwa misimamo ya sera yake ya “Marekani Kwanza” kuwa
inaweza kuharibu uhusiano wa nchi hiyo na bara la Afrika.
Ameyasema
hayo katika mkutano wa dunia wa uchumi World Economic Forum (WEF)
unaofanyika huko Davos nchini Switzerland ambapo amesema kuwa kunatakiwa
kuwepo kwa uwiano wa wenye nguvu kubwa na nguvu kidogo.
Amesema
kuwa Marekani inaweza kupoteza ushawishi wake barani Afrika huku nchi
kama China zinazidi kuimarisha uhusiano na bara hilo kwa kuwekeza katika
sekta mbalimbali.
Bill
Gates anamfuko wake barani Afrika unaoitwa Bill & Melinda Gates
Foundation, ambao umekuwa ukijihusisha kwa kiasi kikubwa kutoa huduma za
afya katika nchi kadhaa.
Hata
hivyo, Rais Trump amesema kuwa atakata msaada wa bajeti ya afya kwa
takribani dola bilioni 2.2 katika mfuko wa dunia, huku akiwakasirisha
viongozi wa Afrika bada ya kuyaita mataifa ya Afrika machafu kupindukia.
0 comments:
Post a Comment