Home » » Rais Magufuli amemteua aliyekuwa Katibu Mkuu Ikulu, Bw. Alphayo Kidata kuwa Balozi

Rais Magufuli amemteua aliyekuwa Katibu Mkuu Ikulu, Bw. Alphayo Kidata kuwa Balozi

Unknown | Thursday, January 11, 2018 | 0 comments
Rais John Magufuli ameteua mabalozi wapya wawili ambao ni Alphayo Kidata na Meja Jenerali Mstaafu, Simoni Mumwi.

Taarifa iliyotolewa leo Alhamisi na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Gerson Msigwa imesema kuwa Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi amesema uteuzi wa Kidata umeanza jana Jumatano Januari 10.

Kabla ya uteuzi huo Kidata alikuwa Katibu Mkuu, Ikulu.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa mabalozi hao wateule watapangiwa vituo vyao vya kazi na kuapishwa baada ya taratibu kukamilika.

Advertisement
==
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

 
Support : Copyright © 2018. AFRICAN NEWS BLOG - All Rights Reserved
Imetengenezwa na Edwin Moshi
Inaendeshwa na AFRICAN NEWS BLOG