Kamanda
wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema
askari wanaotembea na pikipiki maarufu kama ‘tigo’ hawana mamlaka ya
kutoza faini kwa mtu aliyevunja sheria za barabarani.
Amesema jukumu lao ni kumkamata aliyevunja sheria na kumpeleka kwa askari wa usalama barabarani.
“Niwasihi
wananchi, msikubali kutoa hela kwa hao askari hiyo itakuwa ni rushwa.
Fedha unayompa inamfaidisha askari husika na familia yake. Jambo hili
tunalipinga mno,” amesema Mambosasa leo Januari 18, 2018 katika kipindi
cha 360 kinachorushwa na Redio Clouds.
Amesema
kikosi hicho cha pikipiki hakikuanzishwa kwa ajili ya kukamata
wanaovunja sheria barabarani na kuwatoza faini, kwamba askari wa usalama
barabarani ndio wenye jukumu la kutoza faini na kutoa risiti.
“Kikosi
cha pikipiki kilianzishwa kwa ajili ya kuangalia usalama na inapotokea
kosa wanawajibika kumfikisha mhusika kwenye mamlaka inayosimamia usalama
barabarani,” amesema.
Ametoa wito kwa askari wa usalama barabarani kutumia busara wakati wa kuteleza majukumu yao kwa mujibu wa sheria.
“Tunaelekeza
polisi asitafute makosa, asikusimamishe bila kujua kwanini
amekusimamisha halafu anaanza kuhangaika kutafuta kosa. Tunaendelea
kuwaeleza wenzetu kuwa busara inahitajika wakati wa kusimamia sheria,”
amesema na kuongeza,
“Hawapaswi
kuwaumiza watu. Askari unatakiwa kufikiria tu unamtoza faini mtu mchana
kwa kuwa taa zake haziwaki sasa hapo anakuwa amefanya kosa gani maana
ametembea mchana, labda ingekuwa usiku halafu taa haziwaki hapo sawa.
0 comments:
Post a Comment