Mkazi
mmoja wa mkoa wa Mwanza amefariki dunia baada ya kuigonga ndege ya
Fastjet iliyokuwa ikiruka katika Uwanja wa Ndege Mwanza kuelelea jijini
Dar es Salaam.
Kaimu
MKurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Richard
Mayongela amesema tukio hilo la aina yake limetokea jana usiku.
Amesema ndege hiyo ilikuwa njia moja kuelekea jijini Dar es Salaam, kubainisha kuwa mtu huyo ndiye aliyeigonga ndege hiyo.
“Ingawa
ndege ndio ilimgonga mtu huyo ambaye jina lake hatulifahamu, kisheria
mtu au kitu chochote kinachokuwa kwenye njia ya kurukia na kutua ndege
ndiyo kinahesabiwa kuigonga ndege. Ni kama ilivyo kwa treni,” amesema
Mayongela.
Amesema
kabla ya ndege hiyo kuruka, taratibu zote za kiusalama zilifuatwa
ikiwemo kukagua njia kujiridhisha hakuna kitu chochote.
“Haijulikani
mtu huyo alitokea wapi. Vyombo vya ulinzi na usalama vipo eneo la tukio
kuchunguza tukio hilo kwa kina na tutatoa taarifa kamili uchunguzi
utakapokamilika,” amesema kaimu mkurugenzi huyo.
Amesema
kitendo cha mtu huyo kuwepo katika njia ya kurukia ndege licha ya
ukaguzi kufanyika kinawaumiza vichwa viongozi na wataalam wa usalama
uwanjani hapo.
“Pengine
tatizo la muda mrefu la kukosa uzio tunaloanza kukabiliana nalo kwa
ujenzi na upanuzi wa uwanja linaweza kuwa chanzo cha mtu huyo kuingia
katika njia ya kurukia ndege,” amesema.
Ili kukabiliana na matukio ya aina hiyo, amesema wataimarisha mifumo ya usalama kwenye viwanja vya ndege nchini.
0 comments:
Post a Comment