Mbunge
wa Mtama (CCM), Nape Nnauye amehoji sababu za vyama vya siasa
kuhangaika kupokea wanachama wa vyama vingine, badala ya kushughulika na
Watanzania wasio na vyama.
Akizungumza
Jumapili Desemba 31,2017 katika mahojiano na kituo cha televisheni cha
Azam, Nape amesema siku zote amekuwa na msimamo tofauti na wanachama
wanaovihama vyama vyao kwa maelezo kuwa unawajenga wanaohama, si vyama.
"Kama
tunataka kujenga vyama viwe vya kitaasisi ni lazima kuhamahama lisiwe
suala la kawaida. Yaani mtu mpaka anahama watu waseme kweli huyu
alistahili kuhama," amesema Nape.
Amesema,
"Watanzania wapo zaidi ya 50 milioni, wenye uwezo wa kujiunga na vyama
kikatiba wanaweza kuwa zaidi ya 30 milioni, waliopo kwenye vyama
wanaweza wasifike 10 milioni. Kwa nini tunakwenda kuhangaika na
wanachama wa vyama vingine badala ya kushughulika na Watanzania wasio na
vyama. Tushughulike kuwashawishi hawa."
Katika
kipindi hicho, mwenyekiti wa kamati ya uongozi ya Chama cha Wananchi
(CUF), Julius Mtatiro na mwanahabari mkongwe, Dk Gideon Shoo waliungana
na Nape kukosoa vitendo vya wanachama kuvihama vyama vyao.
Kwa mtazamo wao, hamahama ya wanasiasa ni miongoni mwa kasoro zilizojitokeza mwaka 2017.
0 comments:
Post a Comment