Mwenyekiti
wa CHADEMA na Kiongozi Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman
Mbowe amewataka Watanzania kuwa tayari kukosolewa na viongozi wa dini
kwani ndio wanaoliombea Taifa liwe na amani katika kipindi chote tangu
nchi ilipopata Uhuru.
Mbowe
ameyasema hayo jana wakati akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari
kuhusu hali ya kisiasa kwa mwaka 2017, ambapo alisema kila mtu ana
mapungufu katika utendaji wake wa kazi hivyo kila mmoja awe tayari
kupokea ushauri kutoka kwa viongozi wa dini.
“Lakini
viongozi wetu wa dini wana haki ya kusema, wana wajibu wa kusema, hawa
ni watu wanaolea Taifa hili kiroho, huwezi kumshambulia Kakobe kama
unamshambulia mtoto mdogo, hawa wana waumini wana followers (wafuasi) na
hawa ndio kila siku Rais anasema wamwombee, sasa wanamwombea vipi
wakati unawapa masharti?,” alisema Mbowe na kuongeza.
“Sisi
wapinzani tunakosolewa, viongozi tuwe na unyenyekevu wa kukubali mawazo
tofauti tukisemwa, tusijenge chuki katika jamii, vyama vyetu vyote
vinaongozwa na binadamu vinaweza vikakosea, tuwaache viongozi wa dini
wafanye kazi yao, tukikosea waseme.”
0 comments:
Post a Comment