Makamu
wa Rais, Samia Suluhu amewataka viongozi wa Mkoa wa Dar es Salaam
kuanzia ngazi za wilaya, halmashauri kuwa na mpango mmoja wa kuboresha
mazingira ili kujikinga na maafa yatakayotokana na mvua hasa mafuriko.
Mama
Samia amesema hayo leo Ijumaa wakati akifungua mkutano unaokutanisha
wadau wa mazingira wa jiji hili ambao una lengo la kuja na mpango kazi
wa kuondoa majanga hasa mafuriko.
Mkutano
huo ambao umeudhuriwa na viongozi na mawaziri mbalimbali akiwamo Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, January
Makamba, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi,
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na wakuu wa wilaya.
Samia
amesema katika maafa yanayotokea katika jiji la Dar es Salaam kumekuwa
na mipango tofauti katika wilaya zote jambo ambalo sio sawa kwani lazima
kuwe na mkakati wa kunusuru jiji zima.
"Lazima
tuwe na mkakati kabambe wa kufanya usafi wa mifereji na hatuwezi
kusubiri maafa ndio tuanze kufanya kazi ya uokoaji sio sawa kabisa,"
amesema Samia.
Katika
mkutano huo ambao mwenyekiti wake ni Makamba amesema kikao hicho
kitatoka na azimio moja katika kukabiliana na majanga hayo.
0 comments:
Post a Comment